Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akizungumza na Wawakilishi wa
nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC)
(hawapo pichani), wakati kiongozi huyo alipokuwa anafungua Warsha
iliyoandaliwa na SADC kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya
usalama ndani ya Jumuiya hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya
Ramada, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez, na Mkuu wa Kituo cha Tahadhari ya Matukio ya Kiusalama katika
Sekretaireti ya SADC, Habib Kambanga.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto meza kuu) akizungumza na
Wawakilishi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa
Afrika (SADC), wakati kiongozi huyo alipokuwa anafungua Warsha
iliyoandaliwa na SADC kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya
usalama ndani ya Jumuiya hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya
Ramada, jijini Dar es Salaam. Wapili kulia meza kuu ni Mratibu Mkazi wa
Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez. Kushoto ni Mkuu wa Kituo cha Tahadhari ya Matukio ya
Kiusalama katika Sekretaireti ya SADC, Habib Kambanga, na kulia ni Afisa
wa kutoka Umoja wa Mataifa (UN), Rokhayatou Diarra.
Mkuu wa Kituo cha Tahadhari ya
Matukio ya Kiusalama katika Sekretaireti ya Jumuiya ya Maendeleo ya
Kusini mwa Afrika (SADC), Habib Kambanga akizungumza katika Warsha
iliyoandaliwa na SADC kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya
usalama ndani ya Jumuiya hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya
Ramada, jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulifunguliwa na Naibu Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa
na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
(wapili kulia meza kuu) akizungumza katika Warsha iliyoandaliwa na SADC
kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya usalama ndani ya Jumuiya
hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Ramada, jijini Dar es
Salaam. Watatu kulia meza kuu ni Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, ambaye pia alifungua mkutano huo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akisindikizwa na Mratibu Mkazi
wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez (kushoto), pamoja na Mkuu wa Kituo cha Tahadhari ya
Matukio ya Kiusalama katika Sekretaireti ya Jumuiya ya Maendeleo ya
Kusini mwa Afrika (SADC), Habib Kambanga (kulia), mara baada ya Masauni
kufungua Warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na Jumuiya hiyo ambapo
Wawakilishi wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo walijadili masuala
mbalimbali ya usalama. Warsha hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa
Mikutano, Hoteli ya Ramada, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), Mratibu Mkazi wa Umoja wa
Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro
Rodriguez (wanne kulia), Mkuu wa Kituo cha Tahadhari ya Matukio ya
Kiusalama katika Sekretaireti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa
Afrika (SADC), Habib Kambanga (wanne kushoto) wakiwa katika picha ya
pamoja na Wawakilishi wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo mara baada ya
Masauni kuufungua Warsha hiyo iliyoandaliwa na SADC kwa lengo la
kujadili masuala mbalimbali ya usalama ndani ya Jumuiya hiyo. Warsha
hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano, Hoteli ya Ramada, jijini Dar
es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
EmoticonEmoticon