Mkutano
wa Mkuu wa Pili wa Chama cha Kudhibiti Mbu cha Pan African (PAMCA)
umeingia katika siku yake ya pili jijini Dar es Salaam ambapo watafiti
wamewasilisha taarifa zao mbalimbali za utafiti walizofanya katika
maeneo yao kutoka nchi mbalimbali za Afrika ikiwa ni pamoja na ushauri
wa kitaalam wa kupata suluhisho la kumdhibiti na hatimaye kumtokomweza
kabisa Mdudu mbu barani Afrika. Pichani ni Mwanasayansi Mtafiti Kutoka
Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dk Bilali
Kabula akiwasilisha taarifa yake. Mkutano huo wa siku tatu ulianza
Oktoba 6 na utamalizika Oktoba 8, 2015.
Imeandikwa na Father Kidevu Blog
Dk
Kabula kutoka NIMR aliwasilisha taaifa ya utafiti uliofanywa jijini Dar
es salaam kuangalia vinasaba vinavyosababisha usugu wa mbu waenezao
Malaria dhidi ya viuatilifu.
Matokeo
ya utafiti huo yalionesha kuwepo kwa vinasaba vinavyosababisha mbu wa
Malaria kumeng’enya viuatilifu na kufanya kuwa sugu.
Aidha Dk Kabula alisema kuwa na vinasaba vya “KDR” (Knockdown Resistance)vinavyosababisha usugu zaidi ya viuatilifu.
Ili
kudhibiti uenezaji wa vinasaba hivyo, ameshauri matumizi ya viuatilifu
aina ya organophosphates na carbonates badala ya pyrethroid.
“Dawa
nyingi hasa zilizopo nchini ambazo watu huzitumia kupulizia mbu
majumbani haziwaui na badala yake mbu hao kuzirai tu kwa muda flani na
baade kuzinduka na kuendelea tena na kuuma na kueneza maambukizi ya
malaria, hivyo dawa mbadala hazina budi kuanza kutumika kupulizia mbu
majumbani,” alisema Dk Kabula.
Washiriki wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa leo katika mkutano huo katika siku yake ya pili.
Mmoja wa wanasayansi watafiti akichangia mad.