Mgombea ubunge Jimbo la Kibaha
mjini Silivestry Koka kupitia tiketi ya (CCM) wakati wa mikutano yake
ya hadhara ya kampeni wakati akizungumza na wananchi wa maeneo mbali
mbali katika kata mbali za visiga pamoja na kata ya Pangani.
Mgombea
huyo ubunge jimbo la Kibaha mjini akiwa anasawasili katika moja ya
mikutano yake huku akiwa anashangiliwa na umati wa wananchi waliofika
kumpokea kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
Wananchi wakiwa wanafuatilia jambo katika moja ya mikutano hiyo ya hadhara..
……………………………………………..
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
WAFANYABIASHARA ndogo ndogo
katika halmashauri ya mji wa Kibaha wameahidiwa kujengewa soka kubwa la
kisasa kwa ajili ya kuweza kuondokana na usumbufu waliokuwa wanaupata
katika kufanya shughuli mbali mbali za kuuza bidhaa zao lengo ikiwa ni
kuwapa fursa kwa ajili ya kuweza kuleta mabadiliko katika kukuza
uchumi.
Ahadi hiyo imetolewa na Mgombea
ubunge Jimbo la Kibaha mjini Silivestry Koka wakati wa mkutano mikutano
yake ya hadhara ya kampeni wakati akizungumza na wananchi wa maeneo
mbali mbali katika kata mbali za visiga pamoja na kata ya Pangani
Koka amesema kwamba endapo
akichaguliwa na wananchi wake kuliongoza jimbo hilo atahakikisha anaweka
mpango mkakati kwa kushirikiana na halmashauri ya mji ili kuweza
kuwakomboa wafanyabiashara hao kwa kuwajengea soko la kisasa ambalo
litaweza kuwasaidia kwa kisi kikubwa kuendeshea shguhuli zao za
biashara.
Mgombea huyo alisema kwamba
anatambua katika jimbo hilo kuna fursa nyingi za kiuchumi hivyo ujenzi
huo wa soko pindi utakapokamilika utaweza utaweza kubadilisha hali ya
kimaisha kwa wananchi hao kwani wataweza kubuni biashara mbali mbali
ambazo watakuwa wanakwenda kuziuza sokoni hapo.
“Mimi kwa upande wangu napenda
kuona wananhci wa jimbo la Kibaha wanapiga hatua kubwa katika suala zima
la maendeleo, hivyo kitu amabcho nimeshajiwekea na nimeshaanza
kukifanya ni kuhakikisha kwamba kunakuwepo na soko kubwa la kisasa
amablo litaweza kuwajumuisha wafanyabiashara mbali mbali wadogo pamoja
na wale wakubwa lengo ni kukuza uchumumi,”
“Kuna vijana na wakinamama wengi
wamekuwa wakipata usumbufu nah ii yote ni kutokana na kukutowa na eneo
la kudumu amablo limetengwa kwa ajili ya kuendeshea kazi zao, hivyo mimi
lengo langu kubwa pindi nikichaguliwa ni kuwawezesha kwa hali na mali
wananchi wangu kwa kuwaongezea mitaji katika biashara zao ili waweze
kutimiza malengo waliyojiwekea.
Pia Koka alisema kwamaba kwa
sasa bidhaa amabzo zimekuwa zikitoka katika mikoa mingine zimekuwa
zikipelekwa katika soko kuu ya Kariakoo, kitu ambacho alidai kuwa
kinawezekana kwa jimbo la kibaha kuwa na soko lake ili bidhaa zote ziwe
zinauzwa hapo na wananchi wataweza kuondokana na kero ya kwenda
kujinunulia mahitaji yao katika eneo lingine.