Balozi
wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Flaviana Matata, akikabidhi begi kwa
mwanafunzi wa Shule ya Msingi, Nyerere iliyoko Manispaa ya Singida,
Oktoba 7, 2015. PSPF kupitia Sera yake ya kusaidia jamii imetoa msaada
wa mabegi na madaftari kwa shule hiyo na ile ya Chididimo iliyoko nje
kidogo ya Manispaa ya Dodoma
NA K-VIS MEDIA, DODOMA NA SINGIDA
BALOZI
wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Flaviana Matata, ametoa wito kwa
wanafunzi wa shule za msingi Chididimo iliyoko Manispaa ya mji wa Dodoma
na ile ya Nyerere iliyoko mkoani Singida kuwahimiza wazazi wao kujiunga
na Mfuko huo.
Balozi
huyo ambaye pia ni Mwanamitindo wa Kimataifa anayefanyia kazi zake
nchini Marekani, ameyasema hayo kwa nyakati tofauti, wakati akikabidhi
vifaa vya shule kwa wanafunzi hao Oktoba 7, 2015.
“Mimi
kama Balozi wa PSPF, ninatoa wito kwa wanafunzi mliopo hapa, kufikisha
ujumbe huu kwa wazazi wenu, kwani kujiunga na PSPF kuna faida nyingi
katika maisha ya sasa na ya baadae.” Alisema
Alisema, PSPF inatoa mikopo mbalimbali kwa wanachama wake kama vile ya viwanja, mkopo wa elimu, na mkopo wa kuanzisha maisha.
Lakini
pia PSPF inatoa mafao mbalimbali kwa wanachama wa Mpango wa Uchangiaji
wa Hiari, yaani (PSS), ikiwemo, Fao la Uzazi, Fao la Uzeeni, Fao la
Elimu, Fao la Ulemavu na Fao la Ujasiriamali.
“Wazazi
wenu wawe wakulima, wafanyakazi walioajiriwa au kujiajiri wanaweza
kujiunga na PSPF kupitia mpango wa Uchangiaji wa Hiari.” Alifafanua
Balozi huyo.
Naye
Afisa Masoko Mwandamizi wa PSPF, Rahma Jemina Ngassa, alisema moja ya
Sera za Mfuko huo ni kuchangia sekta ya Elimu na msaada huo ni
utekelezaji wa Sera wa kusaidia jamii.
“PSPF
inaamini vifaa hivyo vitapunguza kwa kiasi Fulani changamoto zilizokuwa
zinawakabili wanafunzi hao na hivyo watakuwa kwenye nafasi nzuri ya
ushiriki wa masomo kikamilifu.” Alisema.
Kwa
upande wake, Kaimu Afisa Elimu Manispaa ya Dodoma, Christopher Ligonda,
ameupongeza Mfuko huo kwa kuwajali wanafunzi ambao wazazi wao kwa namna
moja au nyingine ni wanachama au wanachama watarajiwa na hata wanafunzi
wenyewe.
Naye
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nyerere iliyoko mkoani Singida, Yesaya
Ramadhani, ameushukuru uongozi wa PSPF kwa kuwafikiria wanafunzi wa
shule hiyo katika kuwasaidia vifaa hivyo ambavyo ni mabegi na madaftari
kuwa ni kitendo cha kweli katika kusaidia jamii ambayo inakabiliwa na
changamoto mbalimbali.
EmoticonEmoticon