Dr.
Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa
serikali wa kwanza kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Magavana wa
Mashariki na Kusini mwa Afrika baada ya mkutano wa MEFMI .
……………………………………………………………………………………
Na Ingiahedi Mduma -Msemaji Mkuu Wizara ya Fedha Lima – Peru
Katika kipindi hiki cha mikutano
ya mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa, kumekuwa na
mikutano mbalimbali inaendelea hapa nchini Peru. Mikutano hiyo
inaendeshwa na Taasisi mbalimbali zenye utaalamu wa kiuchumi na kifedha.
Akizungumza na waandishi wa habari, katibu Mkuu Wizara ya fedha Dr.
Servacius Likwelile alisema “MEFMI ni chombo kikubwa kwa Afrika
Mashariki na Kusini katika kutoa mafunzo ya usimamizi wa mambo ya uchumi
kwa watendaji wa nchi wanachama.” Aliendelea kusema kuwa katika siku
hizi mbili wamekutana na chombo hicho kwa madhumuni ya kuzungumzia
maendeleo ambayo yanatokana na rasilimali kama vile gesi na madinii na
kutoa mapendekezo ya namna gani Afrika inaweza kusimamia rasilimali
hizo.
Akitoa ufafanuzi katika majadiliano hayo Dr. Likwelile
alisema”Tanzania kuna rasilimali nyingi kama vile gesi ambayo
imegunduliwa Mtwara na kusisitiza kuwa kuna nchi mbalimbali barani
Afrika ambazo zina dhahabu ya kutosha ambayo inaweza kuinua uchumi wa
Afrika kama kutakuwa na utaratibu mzuri wa kuzitumia.
“Lengo kuu la mkutano wa MEMFI ni kuzungumzia shughuli
zinazofanywa na MEMFI ili kuwezesha kupanga namna ya kuboresha uwezo na
kuendesha shughuli zetu katika kuinua uchumi wa Afrika kwani tutahitaji
fedha nyingi kwa ajili ya kuwekeza kwenye miundombinu lakini lazima
tuhakikishe kwamba tunafanya hivyo ili kuhakikisha uchumi wetu unakuwa
imara na kunakuwa na utaratibu wa kuweka akiba kwa ajili ya vizazi
vijavyo, hili ni suala la msingi sana” alisistiza Likwelile.
Likwelile aliongeza kuwa “Vizazi vingi vinatumia rasilimali zote
bila kuangalia utaratibu wawakati ujao kuwa utakuwaje, hivyo katika
kikao hiki tumekubaliana kuanzisha mfuko ambo ni kwa ajili ya kuwekeza
kwa ajili ya matumizi ya baadae (Sovereign Wealth Fund). Masharti ya
mfuko huoyatakuwa ni kama ifuatavyo: (i) Mfuko huo lazima uweze
kuzalisha ajira, (ii)Mfuko huo lazima uwe na misingi imara ya kusimamia
uendeshaji wa shughuli zake,(iii) Mfuko lazima uwe na chombo imara
kinacho kisimamia mfuko huo. (iv) Lazima kuwe na utaratibu ambao unasema
mfuko huu utafanya nini na hautafanya nini.
La msingi kuwe na mfumo wa
kisheria lakini tuangalie rasilimali watu ili kuweza kuhifadhi mfuko
huo. Na namna gani miundombinu itawezakusaidia kuimarisha uchumi ili
uweze kutambuliwa.”
Naye Gavana wa Benki kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu alisema
kuwa,ni muhimu kujua mapato yetu yatokanayo na upatikanaji wa madini
kwani tunaweza kuyatumia vizuri katika kuhakikisha tunatengeneza
miundombinu, kuongeza uwezo wa kuzalisha na baada ya hapo nchi iweze
kuendelea kupiga hatua hata kama madini yatakuwa yamekwisha.
Waziri wa Fedha ni Gavana katika mikutano hii, akifuatiwa na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Servacius
Likwelile ambaye ni Gavana msaidizi kwa upande wa Benki ya Dunia (WB),
aidha Gavana wa Benki kuu Prof. Benno Ndulu ni Gavana msaidizi kwa
upande wa Shirika la Fedha la Kimataifa(IMF).
Hali ya hewa mjini hapa ni baridi, rasharasha na manyunyu ya hapa na pale hasa nyakati za asubuhi.
Imetolewa na:
Ingiahedi Mduma
Msemaji Mkuu
Wizara ya Fedha
Lima – Peru
7/10/2015
EmoticonEmoticon