

Mheshimiwa Benard Membe akitoa
heshima za mwisho wakati wa kuuaga mwili wa marehemu kaka yake Ndugu
Simon Camillius Membe mara baada ya kufanyika ibada ya mazishi huko
Kijijini Rondo tarehe 7.10.2015.


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akiwapa pole wana familia ya Marehemu Simon Kamillius Membe mara baada
ya kuhudhuria ibada ya mazishi iliyofanyika huko Rondi, Lindi Vijijini
tarehe 7.10.2015.

Baadhi ya waombolezaji wakipita
mbele ya jeneza ulimolazwa mwili wa Marehemu Simon Membe aliyefariki
dunia huko India tarehe 3.10.2013,

Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Benard Kamillius Membe akitoa neo la
shukrani kwa viongozi wa serikali, Chama Cha Mapinduzi na wananchi
waliojitoa kwa hali na mali katika kufanikisha mazishi ya marehemu kaka
yake Bwana Simon Kamillius Membe aliyefariki dunia huko India tarehe
3.10.2015.

Maandamano ya kwenda kuulaza mwili
wa Marehemu Simon Membe kwenye nyumba yake ya milele huko kijijini
Rondo katika wilaya ya Lindi.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akiweka udongo kwenye kaburi la Marehemu Simon Membe wakati mwa mazishi
katika Kijiji Rondo huko Lindi .

Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Benard Membe akiweka shada la maua
kwenye kaburi la marehemu mdogo wake ndugu Simon Membe wakati wa mazishi
yake huko Rondo TAREHE 7.10.2015.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akiweka shada la maua kwenye kaburi la Marehemu Simon Kamillius Membe
aliyefariki dunia huko India tarehe 3.10.2015.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
EmoticonEmoticon