MIKUTANO YA MWAKA YA KUNDI LA BENKI YA DUNIA NA SHIRIKA LA FEDHA LA KIMATAIFA WAFANYIKA NCHINI LIMA

October 07, 2015

unnamedn 
Dr. Servacius Likwelile Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali wa katikati akiwa pamoja na Gavana wa Benki kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu kushoto na Bi. Natujwa Mwamba Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania kulia, wakiwa katika mkutano wa chombo kinachotoa mafunzo ya kusimamia mambo ya uchumi (MEFMI) nchini Peru – Lima.
Picha na Eva Valerian
…………………………………………………………………………………………….
Mikutano ya mwaka ya Bodi ya Magavana ya Shirika la fedha la Kimataifa na kundi la Benki ya Dunia kwa mwaka 2015 imeanza rasmi hapa mjini Lima –Peru na kuhudhuriwa na maelfu ya watu kutoka nchi mbalimbali Duniani ambapo kilele chake kitakuwa tarehe 12 mwezi Octoba 2015.
Bodi ya Magavana wa Shirika la Fedha la kimataifa ( Mfuko) na Bodi ya Magavana wa kundi la Benki ( Benki ) kwa kawaida hukutana mara moja kwa mwaka kujadili kazi za Taasisi ambazo ziko chini yao. Mikutano hii ya mwaka huwa inafanyika mwishoni mwa mwezi Septemba na mwanzoni mwa mwezi Octoba. Mikutano hii hufanyika mjini Washington kwa miaka miwili mfululizo na kwa mwaka wa tatu hufanyika kwa nchi mwanachama ambaye amepitishwa kutokanana na viwango vilivyowekwa.
Mikutano hii ya Bodi ya Magavana ilizinduliwa huko Savannah, Georgia, Amerika mwaka 1946 na ikaanza kufanyika mjini Washington DC mwaka huo huo.
Mikutano hii ya mwaka itaambatana pamoja na mikutano ya kimataifa ya kifedha, kamati za fedha, Kamati za maendeleo, kundi la nchi kumi, kundi la nchi ishirini na nne, na makundi mbalimbali ya nchi wanachama.
Aidha katika kuhitimisha mikutano hii, Shirika la fedha la kimataifa, kamati ya mambo ya fedha, Kamati ya maendeleo pamoja na makundi mengine watapata nafasi ya kuwasiliana na kutoa mapendekezo yao ya kipi kifanyike ili kuhakikisha mambo wanayojipangia yanatekelezwa.
Magavana watakitumia kipindi hiki kwa kuzungumzia masuala ya kibiashara na kushauriana. Bodi ya Magavana inatumia kipindi hiki kufanya maamuzi ya ni vipi mambo ya Fedha ya kimataifa yanapaswa kuwa na kukubaliana kuhusu maazimio yao.
Mikutano ya mwaka inakuwa na mwenyekiti ambaye ni Gavana wa Benki na wa Mfuko, na uenyekiti huo unakuwa ni wa kupokezana kati ya wanachama kila mwaka. Kila baada ya miaka miwili inachagua Mkurugenzi mtendaji. Kila mwaka wanachama wapya wowote wanakaribishwa katika Benki na mfuko.
Kwa sababu Mikutano hii ya mwaka inakusanya idadi kubwa ya wanachama kutoka nchi mbalimbali, Shirika la fedha la kimataifa na kundi la Benki ya Dunia inatoa nafasi ya kuwapatia ushauri mkubwa na mdogo, kwa mpangilio wa kuwa na utaratibu maalumu au kutokuwa na utaratibu maalumu alimradi hawavurugi mpangilio uliopo.
Semina mbali mbali zinafanyika na zinaendeshwa na wafanyakazi wanachama kwa waandishi wa habari. Aidha programu za Mikutano ya mwaka zimetengenezwa kwa kuzingatia matakwa ya sekta binafsi, wajumbe kutoka Serikalini na maafisa wakuu wa Mabenki na watumishi wa Mfuko.
Mikutano ya mwaka iliyofanyika nje ya Amerika kuanzia mwaka 1947 hadi 2015.
Mwaka Mahali 1947 London 1950 Paris 1952 Mexico City 1955 Istanbul 1958 New Delhi 1961 Vienna 1964 Tokyo 1967 Rio de Janeiro 1970 Copenhagen 1973 Nairobi 1976 Manila 1979 Belgrade 1982 Toronto 1985 Seoul 1988 Berlin 1991 Bangkok 1994 Madrid 1997 Hong Kong 2000 Prague 2003 Dubai 2006 Singapore 2009 Istanbul 2012 Tokyo 2015 Lima
Magavana wa mikutano hiyo ni Mawaziri wa fedha kutoka nchi mbalimbali, Magavana wa Benki kuu na Makatibu wakuu wa Wizara za fedha.
Mpaka sasa karibu nchi zote zimeshawasili katika mikutano hiyo na hali ya hewa ni mawingu na baridi kiasi. Imetolewa na: Ingiahedi Mduma Msemaji Mkuu Wizara ya Fedha Lima – Peru

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »