NAIBU WAZIRI WA MAJI ATEMBELEA MRADI WA MAJI ZIWA VICTORIA,KAHAMA,SHINYANGA NA KISHAPU

August 21, 2015

ZIARA ya naibu waziri ilianzia kwenye chanzo ca maji kitongoji cha Ihelele, kijiji cha Nyanghomango kwa kugagua chanzo, sehemu ya kutibu maji na kusukuma maji kisha kuongea na wananchi wa kijiji cha Nysnghomango
Aidha alikagua mradi unaoendelea kujengwa wa kupeleka maji miji ya mwadui, Maganzo na Kishapu.



Mradi huu mkubwa wa maji unagharimu shilingi bilioni 254 na una uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 120 kwa siku lakini mpaka sasa unazalisha maji lita milioni 80 tu kwa siku na unahudumia miji ya kahama, shinyanga, Ngudu ,vijiji 55 vilivyopitiwa na bomba.



Kwa mujibu wa kaimu mkurugenzi wa Kashwasa ambao ndiyo waendeshaji wa mradi huu injinia Laurance Wasala amesema Mradi huu ni mkubwa na maji yanatosha kufikisha maji Tabora na miji ya mwadui, mwadui, kagongwa, isaka, Tinde, Nzega na Igunga.



Akiwa kijiji cha Nyanghomango naibu waziri wa maji amewahakikishia wananchi kuwa wizara ya maji inafanya kila linalowezekana likamilishe mradi wa maji katika kijiji hicho ambacho ndiyo chanzo.



Kuhusu mradi wa maji kupeleka maji Kishapu, Mwadui na maganzo ameridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na Kashwasa na amehaidi wizara ya maji itafuatilia fedha wizara ya fedha zilizopitishwa katika bajeti zitumwe Kashwasa kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo.

  Naibu waziri wa maji,  Amos Makalla akiwa katika chanzo cha maji Ihelele wilaya ya Misungwi.
 Naibu waziri wa maji,  Amos Makalla akikagua sehemu ya kutibu na kusukuma maji ihelele kulia kwake ( mwenye shati jeupe) ni kaimu mkurugenzi wa Kashwasa injinia Laurance Wasala.
 Naibu waziri wa maji, Amos Makalla Akihutubia wananchi kijiji cha Nyanghomango.
 Naibu waziri wa maji, Amos Makalla akikagua mradi mradi wa Kupeleka maji Mwadui, maganzo na kishapu. Kulia ni mkuu wa wilaya ya Kishapu wilson Nkambaku.
Naibu waziri wa maji, Amos Makalla akionngea na waandishi wa habari kwenye mradi wa maji Kishapu.

Naibu waziri wa maji Amos Makalla ametembelea mradi mkubwa wa maji toka ziwa victoria na kuyapeleka miji ya Kahama, shinyanga, Ngudu, Kishapu, vijiji 55 na Tabora.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »