Dirisha la usajili kwa vilabu vya Ligi Kuu nchini (VPL), Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) limefungwa jana
ambapo vilabu vitatu tu vya VPL vimeshindwa kuwasilisha usajili wao wa
wachezaji katika muda uliopangwa.
Klabu za Coastal Union ya Tanga, Stand United ya Shinyanga na Toto
African ya jijini Mwanza zimeshindwa kuwasilisha usajili wao wa
wachezaji, faini ni laki tano (500,000) kwa kila klabu iliyochelewesha
usajili au itakayobadili majina au kuongeza majina baada ya tarehe ya
jana.
Awali TFF ilitoa muda wa wiki mbili kwa vilabu vyote nchini
kukamilisha usajili, ambapo vilabu 13 vya ligi kuu vimeweza kukamilisha
ndani ya wakati, vilabu 24 vya ligi daraja la kwanza, vilabu 24 ligi
daraja la pili pia vimeweza kukamilisha usajili wao ndani ya muda
uliopangwa.