Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetuma salam za rambi
rambi kwa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Pwani (COREFA) kufuatia kifo
cha mwamuzi mstaafu wa mpira miguu Rajabu Zarara kilichotokea juzi usiku
jijini Dar es salam.
Marehemu Zarara licha ya kuwa mwamuzi alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Waamuzi mkoa wa Pwani, amezikwa jana jijini Dar es salaam.
TFF pia imetuma salam za rambi rambi kwa Mwenyekiti wa klabu ya
Yanga, kufuatia kifo cha mwanachama wake Athuman Makaranga kilichotokea
leo asubuhi jijni Dar es salaam.
Makaranga alikuwa ni mwanachama wa klabu hiyo miongoni wa wadau wa
mpira wa miguu, ambapo alishiriki vyema kwenye michuano ya Kagame
iliyomalizika hivi karibuni.
TFF kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini inawapa pole
wafiwa, ndugu, jamaa na marafiki wote kufuatia misiba hiyo na kusema iko
pamoja nao katika kipindi hiki cha maombolezo.