Timu ya Taifa ya Wanawake ya Kenya (Harambee Starlets) tayari
imewasili kisiwani Zanzibar ikiwa na kikosi cha wachezaji 17 pamoja na
viongozi 9 tayari kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Twiga Stars siku ya
jumapili.
Mchezo huo wa kirafiki unatarajiwa kuanza majira ya saa 10 kamili
jioni katika Uwanja wa Amani kisiwani Zanzibar, ambapo viingilio vya
mchezo huo itakua ni shilingi elfu mbili kwa jukwaa kuu, na shilingi
elfu moja kwa mzunguko.