OKWI AWALIZA MASHABIKI WA SIMBA TANGA.

March 20, 2015

KITENDO cha Mshambuliaji wa Simba SC Mganda, Emanuel Okwi kushindwa kufunga mabao matatu ya wazi katika mechi ya Ligi kuu soka Tanzania Bara kimewaumiza wapenzi na mashabiki timu hiyo huku wengine wakimwaga machozi.

Tukio hilo lilijitokeza mara baada ya kumalizika kwa mechi ya Ligi kuu
  ya Vodacom Tanzania bara kati yao na Mgambo Shooting amabapo Simba ilikubali Kichapo cha Mabao 2-0, mchezo uliochezwa uwanja wa CCM Mkwakwani.

Mshambuliaji huyo ambaye alianza katika kikosi cha wekundu hao ambacho
  kilianza kwenye mechi hiyo alijikuta akishindwa kuzitumia nafasi za wazi kwenye dakika ya 35 ambapo alipaswa kufunga bao baada ya kushindwa kuunganisha vema pasi ya Hassani Kessy.

Bao la pili ambalo Okwi alishindwa kulifunga ni kwenye dakika ya 47
  ambapo alipata nafasi ya wazi akiwa langoni mwa Mgambo Shooting na kushindwa kucheka na nyavu jambo ambalo liliwakasirisha mashabiki wa timu hiyo.

Halikadhalika tukio jengine ni bao la tatu la wazi la dakika ya 68

alilolikosa Emanuel Okwi kwa kushindwa kuitendea haki nafasi ya wazi aliyoipata baada ya kupewa pasi na Elias Maguli ambaye aliingia dakika ya 46 kuchukua nafasi ya Ibrahimu Ajibu aliyekwenda benchi.
  “Mimi sijui leo Okwi amepatwa na nini yaani ameshindwa kuipa ushindi timu yetu mara mbili hii imeniumiza sana alisikika akisema shabiki huyo ambaye alijulikana kwa jina la Andrew.

Baada ya kushindwa kuonyesha makeke kwenye mechi hiyo, Kocha Mkuu wa
  timu hiyo, Goran Kopunovic alishindwa kuvumilia hali hiyo na kulazimika kumfanyia mabadiliko katika dakika ya 79 na kumuingiza Saimon Sserunkuma.

Kutokana na uamuzi huo wa Kocha huyo, mashabiki wa wapenzi ambao
  walikuwa wamefurika kwenye uwanja huo walianza kumzomea mshambuliaji huyo kwa muda na kuendelea kutazama mechi hiyo mithili ya watu waliokuwa wamekata tamaa.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »