Waziri wa TAMISEMI Mhe.Hawa Ghasia
akijibu swali kwa niaba ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais na Menejimenti
ya Utumishi wa Umma lililoulizwa na Mhe. Yahya Issa (Mb )wa Chwaka
tarehe 20.03.2015.Mjini Dodoma.
…………………………………………………………………………………………
Na Anitha Jonas – MAELEZO,Dodoma.
Serikali imesema inauhitaji wamafundi sanifu 10,000 wa maabara(Laboratory Technicians) mpya zionazojengwa nchini.
Hayo yameyasema na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bungeni
Mjini Dodoma, Mhe.Hawa Ghasia alipokuwa akijibu swali la nyongeza la
Mbunge wa Chwaka, Yahya Kassim
Issa (CUF).
Katika swali lake Issa alitaka kujua kwa nini Serikali huwapa mikatabawatumishi waliostaafu wakati wapo vijana wengi ambao hawana kazi.
Waziri Ghasia alisema Serikali hutoa mikataba kwa baadhi ya kada ambazo bado hazijitoshelezi kutokana na kuwa na wataalamu wachache.
“Kwa mfano kwa sasa Serikali ina mahitaji makubwa wa mafundi sanifu wa
maabara kwa ajili ya kusimamia maabara zetu zinazojengwa walipo kwasasa hawafiki 1,000 wakati mahitaji ni 10,0000,” alisema Ghasia.
Awali akijibu swali la Msingi la Mbunge huyo, Ghasia alisema sio seraya Serikali kuwaajiri wastaafu isipokuwa pale tu inapoonekana ni kwamanufaa ya umma kutokana na mahitaji makubwa katika sekta husika.
Alisema vijana na wasomi waliohitimu vyuo mbalimbali hapa nchini hupatiwa ajira kulingana na mahitaji ya bajeti iliyopo.
Waziri Ghasia alisema Kwa mujibu
wa Kifungu cha 17 (1) cha Sheria ya Pensheni kwa Watumishi wa Umma sura
namba 371, mtumishi wa umma anayo hiari ya kustaafu
kwa hiyari akifikisha umri wa miaka 55.
Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya wakiwa
wamesimama ndani ya Bunge mara baada ya kutambulishwa kwa uwepo
wao,Mjini Dodoma tarehe 20.03.2015.
EmoticonEmoticon