Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Distilleries LTD,David
Mgwassa (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
wakati wa kutangaza kuchangia kiasi cha shilingi milioni 10 kwa Mfuko wa
Imetosha Foundation.Kushoto ni Balozi wa Harakati ya Imetosha,Henry
Mdimu na kulia ni Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network,Joachim Mushi.
Balozi
wa Harakati ya Imetosha,Henry Mdimu akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) kwenye ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO jijini Dar es
salaam leo,wakati wa kutangaza matembezi ya hisani yatakayofanyika Machi
29 kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es salaam na kuongozwa na
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mh. Mathius Chikawe.Wengine pichani
toka kulia ni Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network,Joachim
Mushi,Katibu wa Harakati ya Imetosha,Salome Gregory pamoja na
Mwanamuziki Mkongwe nchini,Jhiko Manyika “Jhikoman”.
Sehemu
ya Wajumbe wa Harakati ya Imetosha waliofika kwenye Mkutano na
Waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar
es salaam,wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Picha na Othman Michuzi
……………………………………………
Kampuni
ya Tanzania Distilleries LTD (TDL),imechangia kiasi cha sh.milioni 10
kwa harakati ya Imetosha inayopiga vita mauaji ya watu wenye
Ualbino,ambayo itafanya matembezi ya hisani machi 29 mwaka huu
yatakayofanyika kuanzia katika viwanja vya Biafra na kuishia katika
Viwanja vya Leaders Klabu,Kinondoni jijjni Dar es Salaam.
Akizunguma
na waandishi wa habari wakati kutangaza kutoa mchango huo,Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni hiyo,David Mgwassa amesema kupinga mauaji ya watu
wenye ulemavu ni jukumu la kila mtanzania,hivyo TDL kama watanzania
wameona umuhimu kuchangia harakati hizo,kwani hata sifa mbaya
zinazopatikana nje ya nchi hazilengi mtu mmoja au kundi fulani.
Amesema
watu wengine wajitokeze kuunga mkono harakati hizo ili kuwa sehemu ya
watu ambao wanaguswa na suala la mauji ya watu wenye ualbino.
Matembezi
hayo yataongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mathias Chikawe
ambapo ujumbe wa serikali utatolewa katika harakati zinazoendelea za
kukomesha mauaji ya watu hao wenye Ualbino.
Akizungumzia
Matembezi hayo,Balozi wa Harakati ya Imetosha,Henry Mdimu amesema
matembezi hayo hayalengi kukusanya fedha wanachohitaji ni watu washiriki
matembezi hayo.
mdimu
amesema kuwa harakati hiyo ni ya kutoa elimu katika mikoa ambayo mauji
ya watu wenye ualbino ili kuweza kubadilisha hali hiyo na isiendelee
kuwepo.
“Hatulengi
masuala ya fedha tunachotaka wananchi wafikishiwe elimu na watu
wanaofanya hivyo washindwe kufanya kutokana na elimu iliyotolewa kuanzia
katika familia”amesma Mdimu.
Amesema
harakati hizo zimetokana na nguvu ya wadau ambao wamejitolea nguvu zao
katika kuweza kukomesha mauaji ya watu wenye Ualbino hapa nchini.