Waziri wa Ardhi,Nyumba na
Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi(kulia)akiwasili kwenye makao makuu ya
halmashauri ya wilaya ya Arusha,iliyopo wilayani Arumeru katika ziara
yake ya siku tatu na ujumbe wake.
Waziri wa Ardhi,Nyumba na
Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi akizungumza na wakazi wa wilaya ya
Arumeru kwenye viwanja vya halmashauri ya Arusha eneo la Sekei,alipata
fursa ya kusikiliza kero za mashamba ambayo aliahidi kuifanyia
kazi,kulia ni Mpima Ramani mkoa wa Arusha,Hamduni Mansoor na kushoto ni
Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Agatha Msuya.
Mzee Alfred Lekshon mkazi wa
wilaya ya Arumeru akimweleza Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya
Makazi,William Lukuvi jinsi alivyonyang’anywa shamba lake lenye ukubwa
hekari 25.
Mkazi wa Olosiva ,wilaya ya
Arumeru mkoa wa Arusha,ambaye ni mjane Mwanahamisi Almasi akisimulia
kero anazozipata kutoka kwa mtu anayetaka kumnyang’anya nyumba na
kiwanja chake na kuwa amekua akisumbuliwa na kutishiwa .
Mwekezaji ambaye kutoka nchini
Denmark,Finn Petersen ambaye kutokana na migogoro ya ardhi ameshindwa
kuendelea na uwekezaji wake eneo la Oljoro baada ya eneo lake kuvamiwa
na wananchi.
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,Juma
Idd(katikati)akifafanua jambo wakati akieleza mpango wa kutekeleza
mradi wa kuliweka Jiji la Arusha katika hadhi ya kimaita
utakaotekelezwa hivi karibuni,kulia ni Mpima Ramani wa mkoa wa
Arusha,Hamduni Mansoor.
Waziri wa Ardhi,Nyumba na
Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi(kushoto)akipata ufafanuzi wa
mojawapo wa majalada kwenye ofisi ya Masjala ya Ardhi kutoka Afisa Ardhi
Mteule wa halmashauri ya wilaya ya Arusha,Rehema Mdee .
Makamu Mwenyekiti wa halmashauri
ya wilaya ya Arusha,Agatha Msuya akizungumza kwenye mkutano wa wananchi
kueleza kero za mashamba na viwanja kwa Waziri wa Ardhi,Nyumba na
Maendeleo ya Makazi.
Meya wa Jiji la Arusha,Gaudence
Lyimo akizungumza na wananchi kwenye viwanja vya Makumbusho ya Taifa
wakati wa mkutano wa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya
Makazi,William Lukuvi kusikiliza kero za wananchi.Picha zote na Muungano
Saguya.
EmoticonEmoticon