Katika
kuhakikisha madereva wanaosambaza bidhaa za kampuni wanafanya kazi zao
kwa ufanisi,kampuni ya TBL Group imeandaa mafunzo maalumu kwa madereva
kutoka viwanda vyake vilivyopo katika mikoa ya Dar es
Salaam,Arusha,Moshi,Mbeya na Mwanza.
Mafunzo hao ambayo yamemalizikia
mkoani Arusha yaliendeshwa na mkufunzi wa madereva kutoka kampuni ya
CFAO Motors,Hubert Kubo ambaye amewapatia madereva hao elimu ya udereva
wa kujihami ikiwemo utunzaji wa vifaa wanavyoviendesha.
Baadhi ya madereva waliohudhuria
mafunzo hayo walishukuru mwajiri wao kwa kuwapatia mafunzo mbalimbali
kuhusiana na kazi yao ambayo walidai yanawawezesha kufanya kazi yao kwa
ufanisi na kuwa na uwezo wa kukabili changamoto mbalimbali za kikazi
kwa urahisi.
Madereva wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na Mkufunzi Hubert Kubo yaliyofanyika Arusha
Madereva wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na Mkufunzi Hubert Kubo yaliyofanyika Arusha
EmoticonEmoticon