Mgeni
Rasmi Tamasha la Ajira na Ujasiriamali Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mh Luhanga Mpina Akikagua Maonyesho
ya Kazi Mbalimbali Kwenye Tamasha la Ajira na Ujasiriamali
Lililofanyika Chuo Kikuu Mzumbe Mkoani Mbeya.
Katika
kutengeneza Msingi Mzuri kwa Wanafunzi wake na kuwajengea uwezo Chuo
Kikuu cha Mzumbe kampasi ya Mbeya kilifanya maonyesho makubwa ya Ajira
na Ujasiriamali siku yatarehe 11 June 2015 mjini Mbeya. Tukio hilo la
aina yake, pia lilishirikisha wanafunzi wa vyuo wingine vya nyanda za
juu kusini.
Afisa Mtendaji Mkuu waEAG group Imani Kajula Akitoa Mada kwenye Tamasha La Ajira na Ujasiriamali Lililofanyika Mkoani Mbeya
Upatikanaji
wa ajira za uhakika imekuwa changamoto kubwa sana kwa vijana wengi
wanaomaliza vyuo Nchini Tanzania hivyo ujasiriamali ni njia moja muhimu
ya kutatua changamoto hiyo.Wanafunzi wengi walioshiriki walieleza Furaha
yao kwa Maonyesho hayo. Mgeni rasmi Mh.Mpina aliwataka Wanafunzi
kutumia fursa zilizopo kujiletea Maendeleo na kujiajiri.
Mkurugenzi
wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba Ambaye naye
alitoa Mada Mbalimbali Namna ya Kukabiliana na Changamoto ya Ajira Hapa
Nchini
Katika
kufanikisha siku hiyo wataalam na wabobeaji wa biashara na fursa za
ajira walialikwa kutoa mada na kushare uzoefu wao kwenye ujasiriamali na
utendaji kazini. Watoa
mada walio alikwa kwenye kongamano hili kubwani; Imani Kajula ambaye ni
Mkurugenzi Mtendaji wa EAG Group, Ruge Mutahaba ambaye ni Mkurugenzi wa
Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group. Wakili Alberto Msando
– Wakili maarufu wa kujitegemea na Mjasiriamali, Victor Kikoti
Compliance Manager – LAPF na Ephraim Lwila – Meneja wa Tawi la CRDB
Mbeya. Mgeni Rasmi wa Kongamano hilo alikuwa Naibu Waziri wa Mazingira
na Muungano Mh.Luhaga Mpina.
Washiriki
wa Tamasha Hilo wakisikiliza Kwa Makini Mda Mbalimbali Zilizowasilishwa
Kwenye Tamasha la Ajira na Ujasiriamali Lililofanyika Chuo Kikuu
Mzumbe Kampasi ya Mbeya
Pia
katika kuhitimisha siku hiyo, Timu za wanafunzi wa Mzumbe Mbeya na TIA
Mbeya walicheza Mechi ya mpira wa miguu, ambapo chuo cha Mzumbe
kiliifunga TIA kwanjia ya penati. Mkurugenzi wa EAG Group Imani Kajula
alikabidhi zawadi kwa timu zote mbil
EmoticonEmoticon