Wanafunzi
kutoka vyuo vikuu vya Tanzania wanaochukua fani ya Teknolojia ya Habari
na Mawasiliano (TEHAMA) wakionyesha vyeti vyao mara baada ya kumaliza
programu ya wiki tatu ya“Seeds for the future” ambayo ilifanyika katika
makao makuu ya Huawei Technologies yaliyopo Shenzhen, China. Programu
hiyo inaendeshwa na kudhaminiwa na Kampuni ya mawasiliano na teknolojia,
Huawei Tanzania.
Wanafunzi
kutoka vyuo vikuu nchini Tanzania wanaochukua fani ya Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wakizungumza na Balozi wa Tanzania nchini
China Mhe. Lt. generali (Mstaafu) Abdulrahaman A. Shimbo katika
ufunguzi rasmi wa programu ya “Seeds for the future” ambapo wanafunzi 10
kutoka Tanzania walipata fursa ya kujifunza kwa vitendo juu ya fani
hiyo ya teknolojia na mawasiliano kwa muda wa wiki tatu, programu
iliyodhaminiwa na kampuni ya mawasiliano na teknolojia, Huawei Tanzania.
Wanafunzi
10 kutoka vyuo vikuu vya hapa nchini wanaochukua fani ya Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wakiwa katika picha ya pamoja
walipotembelea sehemu ya makumbusho katika mji wa Shenzhen nchini China
walipokuwa nchini humo kushiriki mafunzo kwa vitendo kupitia programu ya
Seeds for the Future” inayoendeshwa na kudhaminiwa na kampuni ya
mawasiliano na teknolojia, Huawei Tanzania.
Shenzhen,
China. 08 Juni 2016. Wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya hapa nchini ambao
walikwenda China kuhudhuria mafunzo ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA), wameipongeza Kampuni ya Huawei Tanzania kwa
kuanzisha mradi huo wenye lengo la kuongeza ufanisi kwenye masuala ya
TEHAMA nchini na kuongeza uelewa juu ya katika sekta ya mawasilino na
kuhamasiha ushiriki wa kimataifa katika Teknolojia ya habari na
mawasiliano.
Wakizungumza
wakati wa mahafali baada ya mafunzo ya programu ya Seeds fo the Future"
katika makao makuu ya Huawei Shenzhen nchini China, walisema wanatambua
mchango mkubwa unaotolewa na Huawei ili kuleta maendeleo katika sekta
ya teknolojia ya habari na mawasiliano nchini Tanzania.
Mwanafunzi
kutoka Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA), Ahmed Sufiani Makame (22)
alisema mafunzo waliyopata yamewawezesha kufahamu teknolojia mpya kabisa
ambayo awali hawakuwa nayo na hawakuipata katika vyuo vya nchini
Tanzania, jambo lililowapa changamoto ili kuweza kukabiliana na
mabadiliko yaliyopo katika sekta ya ajira watakapoajiriwa hapo baadaye.
"Alisema
katika karne hii ya 21 waajiri huhitaji wafanyakazi ambao wanauzoefu wa
kutosha na elimu bora. Wanahitaji waajiriwa wao wawe na ujuzi na
mtazamo chanya. Ninashukuru sana Huawei kwa kutupa nafasi ya kuvumbua
mapya katika ulimwengu wa teknolojia.
Alisema
kutokana na mafunzo waliyoyapata nchini China, kwa sasa wamepata ujuzi
ambao watautumia kutatua changamoto zilizopo zilizopo kwenye kampuni za
mawasilino nchini Tanzania. Aliongeza kuwa, kupitia elimu masafa
(e-learning), usalama wa mitandao, mpangilio wa miji, mifumo ya mtandao,
3G, 4g, mifumo ya data serikalini na hospitali ni mojawapo ya vitu
ambavyo vitaifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zilizopiga hatua
kimaendeleo katika sekta ya TEHAMA.
"Wakati
wa mafunzo yetu China, tuliona ni namna gani Huawei imejipanga na
mabadiliko ya kiteknolojia wakiwa na kaulimbiu yao 'ulimwengu
uliounganishwa'. Mafunzo tuliyoyapata yametupa mwanga kuzishauri kampuni
za mawasiliano pamoja na serikali kuwa wanapaswa waendane na maendeleo
ya teknolojia ya kisasa ulimwenguni," alisema.
Alisema
amepata uzoefu wa mifumo ya 3G NA 4G na mifumo inayotumika kwenye
kompyuta na namna ya kuzitengeneza na kuingiza huduma ya HSI,VolP na
IPTV, siyo tu kwa kujifunza kwa nadharia bali pia ameweza kuitumia kwa
vitendo.
Kwa
mujibu wa Meneja Uhusiano wa Huawei, Jimmy Liguo alisema "Programu ya
Seeds for the Future" inaendeshwa ulimwenguni kote. Miongoni mwa miradi
ambayo Huawei imeipa kipaumbele ni huo na itaendelea kuwekeza kwa muda
mrefu kwenye programu hiyo.
"Programu
hiyo ilianzishwa na Huawei mwaka 2008 kwa lengo la kukuza uelewa katika
masuala ya TEHAMA, kuimarisha sekta ya mawasiliano, kuhamasisha
ushiriki katika jamii ya kidijitali," alisema.
Mwaka
2008 Huawei ilizindua programu kuwaendeleza wataalamu ambao
wanahitajika kwa haraka ili kuendeleza sekta teknolojia ya habari na
mawasiliano katika nchi ambazo Huawei inafanya kazi zake. Huawei
imeazimia kuwezesha mafunzo ambayo yataimarisha elimu inayotolewa
darasani iendane na mahitaji halisi katika sekta ya TEHAMA ili elimu
hiyo iwe endelevu.
Alisema
katika nchi nyingi, bado kuna tatizo la mafunzo yanayotolewa
hayaendania na kile kinachohitajika katika soko la ajira ulimwenguni,
Hivyo watu wenye ujuzi wanatakiwa kupewa fursa za mafunzo zaidi ili
kuweza kuitumia teknolojia ya kisasa.Kupitia Mradi wa Seeds for Future"
Huawei imewezesha kutatua tatizo hilo.
EmoticonEmoticon