Mchezo
wa SAKASAKA unaoendeshwa na kituo cha EFM redio umeanza rasmi siku ya
jumapili ya Juni 12,2016 pale viwanja vya Mcanada, Tegeta ukiwahusisha
wakazi wa wilaya ya Kinondoni.
Kiasi
cha shilingi milioni 3 taslimu zimetolewa kwa washindi 12 ambapo mshindi
wa kwanza aliondoka na milioni mbili, wapili na watatu laki mbili,
mshindi wanne hadi wasita laki moja na washindi sita wa mwisho kupata
elfu hamsini kila mmoja.
Baadhi ya picha za washiliki wakisaka kitu kilichofichwa.
Umati wa watu waliohudhuria sakasaka katika viwanja vya Mcanada,Tegeta.
Mtangazaji
wa Efm radio katika kipengele cha Fimbo chapa kinachosikika katika
kipindi cha joto la asubuhi, Chogo akimuhoji mmoja wa washiriki wa
mchezo huo.
Meneja matukio na mawasiliano Neema Godlays Mukurasi (kushoto) akimkabidhi mshindi mmojawapo wa sakasaka.
Mshindi wa kwanza Rashid Saleh Sengela (katikati) akisubili kupokea pesa yake baada ya kushinda shilingi milioni mbili taslimu.
Washiriki
waliojipatia vitu vyao wakisubiria kuhakikiwa kama ni vya ushindi ama
la ambapo miongoni mwao walijinyakulia pesa taslimu kutoka EFM radio.
EmoticonEmoticon