Shirika
la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF limefanya semina na kuzindua mpango
wa kuwaandikisha madereva wa Bodaboda Mkoani Dodoma, Mpango huo
ulifanywa kwa ushirikiano wa Manispaa ya Mji wa Dodoma, VETA , Trafiki
Mkoa na NSSF umezinduliwa na Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,
Ajira,Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama.
Pamoja
na Uzinduzi wa Uandikishaji Waziri Jenista Mhagama aliwapatia Vifaa vya
Usalama Madereva hao wa BodaBoda Mkoani Dodoma vifaa hivyo ni Kofia ya
Usalama na Kikoti Maalumu cha Usalama ambavyo vimeandikwa Namba
kulingana na Kituo cha Bodaboda Wanachofanyia Kazi. Pia Waziri amezindua
mfumo wa kuvipa namba na kuviweka alama Vibao vituo vyote vya Bodaboda
mkoani Dodoma.
Mkurugenzi
Mkuu wa NSSF Prof. Godius Kahyarara akiongea na Madereva wa Bodaboda
(hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi rasmi wa Kampeni ya Kuandikisha
Madereva wa Bodaboda Mkoani Dodoma.
Waziri
wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira,Vijana na Watu wenye Ulemavu
Jenista Mhagama akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Mpango wa kuwaandikisha madereva wa Bodaboda Mkoani Dodoma.
Meneja
wa NSSF Mkoa wa Dodoma Rehema Chuma akitoa elimu kwa Madereva wa
Bodaboda wa Mkoa wa Dodoma waliouzulia zoezi la uzinduzi wa kampeni
rasmi ya kuwatambua na kuwaandikisha NSSF madereva wa Bodaboda.
Waziri
akikabidhi moja ya pikipiki ambazo wamekopeshwa madereva wa Bodaboda
Dodoma na Manispaa ya Dodoma. Wakishuhudia ni Mwakilishi wa Kamanda wa
Trafiiki Mkoa, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF na
Mkuu wa Chuo cha VETA Dodoma.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu
Jenista Mhagama akimvalisha mmoja wa Madereva wa Bodaboda Kofia Ngumu ya
Usalama iliyotolewa na NSSF. Anayeshuhudia kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof, Godius Kahyarara.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu
Jenista Mhagama akimvesha Jaketi maalumu la Usalama Dereva wa Bodaboda
Mkoa Dodoma akimsaidia Waziri ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye ni
Mkuu wa Wilaya ya Bahi Francis Mwonga.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu
Jenista Mhagama akikabidhi mfano wa Kituo Cha Bodaboda kwa Mwenyekiti
wa Bodaboda Mkoani Dodoma Bang'ara Lucas Kang'alo akishuhudia katikati
Mkurugenzi wa NSSF Prof Godius Kahyarara.
Mwenyekiti
wa Bodaboda Mkoa wa Dodoma akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa
Nchi Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama,
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye ni Mkuu wa Wilaya wa Bahi
Francis Mwonga( Wa Kwanza kulia kwa Waziri), Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,
Prof Godius Kahyarara (Kushoto kwa Waziri) na Mkuu wa Chuo cha Veta
Dodoma Bw. Mattaka baada ya kupokea mfano wa kadi ya Mwanachama ya NSSF
akiwa mmoja ya wanachama wapya waliojiunga NSSF.
EmoticonEmoticon