MKUTANO MKUBWA WA OYES 2016 WAANZA KATIKA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA

June 13, 2016
Umati wa wananchi wa Jiji la Mwanza ukifuatilia mahubiri ya Mwimbaji na Mhubiri JJ.Rwiza wakati akihubiri jana katika ufunguzi wa Mkutano wa Open Your Eyes and See OYES 2016 unaofanyika katika Viwanja vya Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza.

Mkutano wa OYES 2016 ulianza jana June 12,2016 na unatarajia kufikia tamati jumapili ijayo June 19,2016 ambapo kila siku utakuwa ukianza majira ya saa nane mchana. Ni Mkutano mahususi kwa ajili ya kuwafungua watu wote wenye uhitaji ambao kwa muda mrefu wameteseka na vifungo vya ibirisi.
Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola (Kushoto), akimkaribisha Mwimbaji na Mhubiri JJ.Rwiza kuhubiri katika Mkutano wa Open Your Eyes and See OYES 2016.
Mwimbaji na Mhubiri JJ.Rwiza akihubiri katika Mkutano wa Open Your Eyes and See OYES 2016 unaofanyika Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »