Na Princess Asia, DAR ES SAALAM
SIMBA SC imetupa ndoana zake kwa Emery Bayisenge wa APR ya Rwanda, lakini kumpata kazi ipo.
Bayisenge, beki hodari wa kati mwenye umri wa miaka 21 tu, ni tegemeo la Rwanda kuelekea michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika CHAN mwakani, inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.
Kwa sababu hiyo, Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA) halitapenda kukipoteza kisiki hicho kabla ya CHAN ya mwakani, ambayo wao watakuwa wenyeji.

Simba SC inamtaka Emery Bayisenge, lakini kikwazo ni FERWAFA inayotaka kumtumia katika CHAN mwakani |
Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ni shabiki mkubwa
wa beki huyo na BIN ZUBEIRY inafahamu yuko katika jitihada kubwa za
kuhakikisha anamhamishia Msimbazi.
Bayisenge mwenyewe kwa mvuto wa maslahi na hamu yake kubwa ya kucheza Tanzania, yuko tayati kutua Simba SC- lakini FERWAFA ndiyo kikwazo.
Bayisenge ambaye kabla ya APR alichezea Amagaju na Isonga, amekuwa akiichezea Amavubi tangu mwaka 2011.
CHAN ijayo inatarajiwa kufanyika Rwanda kuanzia Januari 16 hadi Februari 7 ikishirikisha jumla ya timu 16.

EmoticonEmoticon