WANAHABARI NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA DAR ES SALAAM KUJADILI CHANGAMOTO ZA NCHI ZAO

May 14, 2015

 Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua kongamano la kujadili mchango wa vyombo vya habari katika kuimarisha demokarasia na mambo mbalimbali yanayogusa jumuiya hiyo Dar es Salaam leo
 Mwenyekiti wa Shirikisho la Wafanyabiashara wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Felix Mosha akizungumza katika kongamano hilo.
 Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo, Assa Mwambene akijibu maswali ya wanahabari.
 Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga, akizungumza katika kongamano hilo.
 Wapiga picha za habari wakichukua matukio mbalimbali kwenye kongomano hilo.
 Viongozi wakiwa mbele.
 Wadau wa habari wakiwa kwenye mkutano huo.
 Wimbo maalumu wa Jumuiya hiyo ukiimbwa.
Waziri Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na 
wadau wa habari.
............................................................................

Na Dotto Mwaibale

WANAHABARI wa Jumuia ya Afrika Mashariki wametakiwa kukaa pamoja na kuunda sera moja itakayowasaidia kupata habari kutoka pande zote za ukanda huo bila kizuizi.

Mwito huo ulitolewa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Harrison Mwakyembe wakati akifungua kongamano la kujadili mchango wa vyombo vya habari katika kuimarisha demokarasia na mambo mbalimbali yanayogusa jumuia hiyo Dar es Salaam leo.


"Ni jukumu lenu nyinyi wenyewe wanahabri muliopo ndani ya jumuia hii kuanzisha sera moja itakayo wasaidia muweze kufanya shughuli zetu katika nchi yoyoye ya jumuia bila kuzuiliwa" alisema Mwakyembe.

Dk. Mwakyemba alisema serikali haiwezi kuanzisha sera hiyo bali wenye nguvu ya kufanya jambo hilo ni wanahabari wenyewe hivyo ni vema sera hiyo ikiandaliwa waipeleke serikali ili kutengenezwa sheria itakayowapa uhuru waandishi wa jumuia hiyo kufanyakazi zao bila ya kuwekewa na kipingamizi.

bado haina nguvu katika kutetea uhuru wa mwandishi kupata habari  afrika mashariki bila kuzuiwa hivyo ipo haja ya wahusika kupeleka hoja katika serikali zote ili kupatiwa mianya ya kuweka sheria itakayomlinda mwandishi kupata habari nchi yeyeote afrika mashariki bila kizuizi.

 Mwakyembe ameviomba  vyombo vya habari vya Afrika Mashariki kuendelea kuiboresha sekta ya habari na kuwa wabunifu ili kuweza kukuza demokrasia na maendeleo ya nchi zinazounda jumuia hiyo.

Kongamano hilo la siku moja lilihudhuriwa na wanahabari kutoka jumuia hiyo pamoja na wamiliki wa vyombo vya habari. (Imeandaliwa na mtandao wa http://www.habarizajamii.com/)

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »