Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mh. Dkt. Seif Rashid ameipongeza Hospitali
ya Taifa Muhimbili kupitia Idara yake ya Tiba na Upasuaji Moyo kwa
kufanikisha matibabu ya moyo kwa wagonjwa 24 katika kipindi cha siku
nne.
Hayo
ameyasema alipotembelea Hospitali hiyo kuona namna ambavyo wataalam wetu
kwa kushirikiana na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Prince Sultan
Cardiac Centre iliyoko Riyadhi nchini Saudi Arabia ambao wamekuwepo
Muhimbili toka tarehe 9 Mei na wanatarajiwa kuondoka tarehe16 Mei, mwaka
huu.
Dkt.
Rashid amesema ni mfanikio makubwa sana ambayo tumefikiwa hadi hivi sasa
katika upasuaji moyo na tunatarajia kasi hii ya ushirikiano ikiendelea
tutapunguza kwa kasi sana wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa ajili ya
matibabu.
“Kama
ndani ya siku nne tu mmeweza kuziba matundu ya moyo kwa watoto 12 bila
kufungua kifua na mkaweza kufungua vifua vya watoto wengine 12 ambao
kutokana na hali zao walihitaji kufunguliwa vifua, mmenipa moyo sana
kwamba mmejidhatiti kuhakikisha Watanzania wanapata huduma hii kwa
haraka na kwa ufanisi wa hali ya juu, nawapongezeni sana” amesema Dkt.
Rashid.
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akiwa na mtoto ambaye
anasubiri kufanyiwa uchunguzi wa kina kama anahitaji upasuaji wa moyo
au la.
mtoto Catherine Gwabala (6) alikuwa wodini jumamosi iliyopita akisubiri kufanyiwa upasuaji.
Mh.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akimjulia hali leo
baada ya kufanyiwa upasuaji. Kushoto kwake ni mama Catherine akifurahia
baada ya mtoto wake kufanyiwa upasuaji.
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid ambapo kulia kwake ni
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Hussein
Kidanto wakiwa ndani ya Chumba chenye mtambo wa Cath Lab ambao unatumika
kuzibua mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye moyo iliyoziba na pia
mtambo huu pamoja na mambo mengine umetumika kwa mara ya kwanza kuziba
matundu ya moyo bila kufungua kifua. Mtoto huyu ambaye jina lake
limehifadhiwa anasubiri kuzibwa tundu kwenye moyo wake kwa kutumia
mtambo wa Cath Lab. Ndani ya siku tatu ataruhusiwa kwenda nyumbani.
Hapa
ni ndani ya chumba chenye vifaa vya kisasa kabisa kwa ajili ya
wagonjwa wenye kuhitaji uangalizi maalumu (ICU) ambapo mtoto
aliyefanyiwa upasuaji anaangaliwa.
Jopo la wataalam wakiwa ndani ya chumba cha kisasa cha upasuaji moyo wakiendelea na upasuaji moyo.
Jopo la Watalaam wakifurahi baada ya kumaliza upasuaji kwa ufanisi na mgonjwa kupelekwa chumba maalumu (ICU).
Mtoto
Cherish Chatama akifurahi baada kusalimiwa na Mh. Waziri wa Afya na
Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid ambapo pembeni yake ni mama Cherish
Mtoto
Michelle Colila (5) akifurahi baada kusalimiwa na Mh. Waziri wa Afya na
Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid ambapo pembeni yake ni mama Michelle.
EmoticonEmoticon