Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali mtoto Habiba Khalfan
Lipande(6) ambaye amefanyiwa tiba ya kuziba tundu lililokuwa katika moyo
wake kwa kutumia teknolojia mpya bila upasuaji wa kifua katika
hospitali ya taifa Muhimbili.Mtoto Habiba kutoka katia kijiji cha
Mavumba Mkoani Morogogoro ni mmoja kati wa watoto zaidi ya 70
watakofaidika na tiba ya moyo ikiwemo ya kuziba matundu bila ya upasuaji
na ile ya kawaida ya upasuaji Katika Hospitali ya Taifa Muhimbili
Kitengo cha Moyo inayoendeshwa kwa ufadhili ya shirika Al Muntada lenye
makao yake makuu jijini London Uingereza na kufanya shughuli zake nyingi
katika nchi ya Saudi Arabia.Rais Kikwete amewashukuru na kuwapongeza
madaktari hao kwa kazi nzuri na kuwaomba kufanya zoezi hilo kuwa
endelevu(picha na Freddy Maro)
EmoticonEmoticon