Mwanamziki
Ommy Dimpoz ameyasema hayo leo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM
alipokuwa anautambulisha wimbo wake wa Wanjera ambao mrembo Wema Sepetu
amecheza kama Wanjera kwenye video wa wimbo huo na kushiriki kupiga
picha za kuutangaza wimbo huo.
Ommy
alisema haoni kama kuna tatizo lolote kati yake na swahiba wake huyo
licha ya Diamond kutoandika chochote kuhusiana na wimbo huo kama ambavyo
amekuwa akifanya kwa wasanii wengine.
“Labda
hajaposti yupo busy na simu yake, hata mimi kuna vitu vingine huwaga
anaposti na mimi vinanipita pia,” amesema Ommy. “Kwahiyo huwezi ukasema
hajaposti kwa sababu fulani na fulani. Diamond si yuko na Zari au?
Kwahiyo hawezi tena akawa anafocus kwa mambo ya Wema. Wala hawezi
kunimind mimi kwa sababu kamuona Wema, haiwezekani. Halafu kumbukeni
shemeji yetu Zari ni mjamzito msitake kuwatia watu pressure.”