• WATU WATATU WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAJARIBU KUFANYA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA KWA MFANYABIASHARA WA MADINI

March 14, 2015

index 
WATU WATATU WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAJARIBU KUFANYA UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA KWA MFANYABIASHARA WA MADINI AINA YA DHAHABU WILAYANI CHUNYA.
 WALINZI WAWILI WA CITY PUB JIJINI MBEYA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUMSHAMBULIA NA KUMJERUHI MFANYABIASHARA MMOJA MKAZI WA ISANGA.
 MWANAMKE MMOJA AMBAYE HAJAFAHAMIKA JINA WILA MAKAZI YAKE ANATAFUTWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUTUPA MTOTO CHOONI MWENYE UMRI WA SIKU MOJA.
 WATU WANNE WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUINGIZA BIDHAA NCHINI BILA KIBALI.
 JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MWANAMKE MMOJA MKAZI WA ILEMI JIJINI MBEYA AKIWA NA POMBE YA MOSHI NUSU LITA.
 JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAKIWA NA VIPANDE SITA VYA MENO YA TEMBO.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTU MMOJA AITWAE ROBERT MBUKWA (50) MFANYABIASHARA YA MADINI AINA YA DHAHABU NA MKAZI WA MIANZINI WILAYANI CHUNYA ALIVAMIWA NA VIJANA WATATU WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAKIWA NA SILAHA MOJA BUNDUKI AINA YA SHOT GUN 12 BORE YENYE NAMBA 64943 ILIYOTENGENEZWA KATIKA KIWANDA CHA WEMBLEY @ SCOTT LTD KILICHOPO BIRMINGHAM ENGLAND NA KUFYATUA RISASI MOJA HEWANI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 13.03.2015 MAJIRA YA SAA 20:00 USIKU HUKO KATIKA MTAA WA MIANZINI, KATA YA BWAWANI, TARAFA YA KIPEMBAWE, KATIKA MJI MDOGO WA MAKONGOLOSI, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, MHANGA BAADA YA KUYAONA MAJAMBAZI HAYO ALIPIGA KELELE NA KUPATA MSAADA KUTOKA KWA MAJIRANI HALI ILIYOPELEKEA MAJAMBAZI HAYO KUTUPA SILAHA NA KUTOKOMEA KWENYE SHAMBA LA MAHINDI.
BAADA YA KUIPATA BUNDUKI HIYO NA KUIKAGUA ILIKUTWA IKIWA IMEKATWA MTUTU NA KITAKO. AIDHA ENEO LA TUKIO LIMEOKOTWA GANDA MOJA LA RISASI. UPELELEZI ZAIDI WA TUKIO HILO UNAENDELEA IKIWA NI PAMOJA NA MSAKO MKALI WA KUYATAFUTA MAJAMBAZI HAYO.
KATIKA TUKIO LA PILI
WALINZI @ MABAUNSA WAWILI WA CITY PUB ILIYOPO JIJINI MBEYA WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA 1. GOODLUCK KAGALI (23) MKAZI WA ILOMBA NA 2. MAHAMUD MUINGA (25) MKAZI WA ILOMBA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA BAADA YA KUMSHAMBULIA KWA KUMPIGA NGUMI NA MATEKE NA KISHA KUMPIGA NA KITU KIZITO MGUU WA KULIA MFANYABIASHARA MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA BAHATI SANDE (32) MKAZI WA ISANGA NA KUSABABISHA MGUU HUO KUVUNJIKA.
TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO MAJIRA YA SAA 01.00 HUKO KATIKA CITY PUB, KATA YA RUANDA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA, CHANZO CHA TUKIO HILO NI MZOZO ULIOTOKEA BAINA YAO NA MFANYABIASHARA HUYO. WATUHUMIWA WAMEKAMATWA NA MHANGA AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MWANAMKE MMOJA AMBAYE BADO HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE ANATAFUTWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUTUPA CHOONI MTOTO MCHANGA MWENYE UMRI WA SIKU MARA BAADA YA KUJIFUNGUA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 13.03.2015 MAJIRA YA SAA 22:30 USIKU HUKO ENEO LA MLIMARELI, KATA YA UTENGULE –USONGWE, TARAFA YA BONDE LA USONGWE, WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, MSAMALIA MWEMA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA JAPHET SANGA (41) MWALIMU NA MKAZI WA MLIMARELI ALIGUNDUA KUTUPWA KWA MTOTO HUYO MCHANGA NDANI YA SHIMO LA CHOO CHA NJE KATIKA NYUMBA ANAYOISHI YEYE NA WAPANGAJI WENZAKE BAADA YA KUSIKIA SAUTI YA MTOTO HUYO AKILIA.
MTOTO HUYO MWENYE JINSI YA KIKE AMEOKOLEWA AKIWA HAI KWA USHIRIKIANO KATI YA JESHI LA POLISI NA WANANCHI NA AMELAZWA KATIKA HOSPITALI TEULE YA IFISI KWA MATIBABU/UCHUNGUZI ZAIDI. UPELELEZI WA TUKIO HILI UNAENDELEA IKIWA NI PAMOJA NA KUMTAFUTA MTUHUMIWA WA TUKIO HILI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI KUACHA TABIA YA KUTUPA WATOTO KWANI NI KITENDO CHA KINYAMA, KINYUME CHA MAADILI NA NI KINYUME CHA SHERIA ZA NCHINI. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI [MAMA WA MTOTO HUYO] AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA TUKIO LA NNE:
WATU WANNE WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. ZULFUA ABUBAKAR (30) KONDAKTA WA BASI LA KAMPUNI YA TAQWA NA MKAZI WA DSM 2. CHRISTOPHER FREDY (28) MFANYABIASHARA, MKAZI WA MKOMBOZI TUNDUMA 3. EMANUEL MWASHAMBWA (35) MKAZI WA MPEMBA NA 4. STEPHEN KALINGA (29) MKAZI WA MPEMBA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA KOSA LA KUINGIZA BIDHAA NCHINI BILA KIBALI.
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 13.03.2015 MAJIRA YA SAA 09:30 ASUBUHI WAKIWA NA MAZIWA AINA YA LACTOGEN DAZANI 24, SAWA NA KOPO 1,032 YENYE UJAZO WA GRAM 400 KILA MOJA. THAMANI HALISI YA BIDHAA HIZO NI TSHS 17,000,000/=.
AIDHA BIDHAA HIZO AMBAZO ZILIKUWA ZIKIINGIZWA NCHINI BILA KULIPIA USHURU KUTOKA NCHINI AFRIKA KUSINI, KUPITIA NCHINI ZAMBIA KWA NJIA ZA PANYA.
KATIKA TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA MSAKO WA KWANZA, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MWANAMKE MMOJA MKAZI WA ILEMI JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA EDITHA JOHN (34) AKIWA NA POMBE YA MOSHI UJAZO WA NUSU LITA .
MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 13.03.2015 MAJIRA YA 12:00 MCHANA HUKO KATIKA MTAA MAPELELE, KATA YA ILEMI, TARAFA YA SISIMBA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KATIKA MSAKO WA PILI, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. NEHEMIA EMANUEL (22) MKAZI WA KIJIJI CHA MATUNDASI AMBAYE ALIKUWA AKIENDESHA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.622 BJV AINA YA SANLG AKIWA AMEPAKIA ABIRIA WAWILI KATIKA PIKIPIKI HIYO MMOJA WA ABIRIA HAO AKIFAHAMIKA KWA JINA LA MAHENGULA BONIFACE (30) MKAZI WA MSWISWI NA MWINGINE AMBAYE ALIRUKA NA KUKIMBIA BAADA YA KUWAONA ASKARI WAKIWA NA MENO YA TEMBO VIPANDE SITA [06].
WATUHUMIWA WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 13.03.2015 MAJIRA YA SAA 13:00 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAHANGO-MSWISWI, KATA NA TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA.
WATUHUMIWA HAO WALIKAMATWA BAADA YA KUSIMAMISHWA NA KISHA KUPEKULIWA NA NDIPO KATIKA PIKIPIKI HIYO KULIKUTWA MFUKO WA SANDARUSI AMBAO NDANI YAKE KULIKUWA NA MENO HAYO YA TEMBO.
Imesainiwa na: [AHMED Z. MSANGI – SACP] KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »