Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (wa pili kushoto), akipata maelezo
kutoka kwa Mhandisi wa Kampuni ya Delmonte (T) Ltd, Theophile Kireo
(mwenye kofia), ambayo kampuni yake inakarabati barabara ya Mwai Kibaki
eneo la Msasani Dar es Salaam jana. Wengine ni Wataalamu wa barabara
Manispaa ya Kinondoni.
Mhandisi wa Kampuni ya Delmonte (T) Ltd, Theophile Kireo (mwenye kofia wa pili kulia), akitoa maelezo kwa DC Makonda.
DC Makonda (wa kwanza kushoto), akizungumza na wakazi wa Msasani kuhusu kuzingatia usafi wa mazingira.
DC Makonda akikagua mitaro inayojengwa na Kampuni ya Delmonte (T) Ltd.
DC Makonda akiangalia mfereji unaotiririsha maji taka kutoka Hospitali ya TMJ.
Fundi bomba wa Hospitali ya TMJ, Mansoul Mramba akitoa maelezo kwa DC Makonda kuhusu utiririshaji wa maji taka hayo.
DC Makonda (wa pili kulia akinagalia maji taka eneo la Msasani karibu na Ofisi za Tanesco Wilaya ya Kinondoni.
Na Dotto Mwaibale
MKUU
wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda ametoa siku saba kwa uongozi wa
Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam kuacha
kutiririsha maji taka kwenyenda barabarani na kwenye makazi ya watu.
Agizo
hilo amelitoa leo jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya
kushitukiza ya kukagua barabara, madaraja na miundombinu eneo la Msasani
ambalo kwa muda mrefu limekuwa likikumbwa na mafuriko ya mara kwa mara
hasa wakati wa mvua za masika.
"Natoa
siku saba kwa uongozi wa Hospitali ya TMJ kuhakikisha wanaacha
kutiririsha maji taka kutoka katika hospitali hiyo kinyumbe cha agizo
langu zitafuata hatua kali za kisheria" alisema Makonda.
Katika
hatua nyingine Makonda aliwataka wakazi wa eneo hilo la Msasani kuacha
kutupa takataka kwenye mitaro ambazo zimekuwa zikichangia kwa kiasi
kikubwa kuziba kwa mitaro hiyo na kuwa mtu yeyote atakayebainika akitupa
taka taka hizo atachukuliwa hatua kali.
Makonda
alisema Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kujenga na kutengeneza
barabara lakini watu wachache wamekuwa wakiharibu kwa kutupa taka taka
hovyo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)