Salim
Mohammed,Tanga.
,POLISI Wilayani Korogwe Mkoani
Tanga, wamemkamata kondakta wa basi, Abdalla Kayomba (37) ambaye anasadikiwa
kuwa ndie msafirishaji mzoefu wa mihadharati aina ya mirungii kati ya
Kilimanjaro na Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kaimu kamanda wa polisi Mkoani
Tanga, Juma Ndaki, alisema tukio hilo lilitokea januari 29 saa 6 usiku kwenye kizuizi
cha polisi kijiji cha Chekelei Tarafa ya Mombo Wilayani Korogwe.
Alisema
wakati wa kukamatwa kwake kijana huyo
alikutwa na kilo 35 za mirungi ambayo alikuwa ameificha chini ya uvungu wa lori
na kuweka katika magunia mawili ya mkaa .
“Kwanza
baada ya polisi kumuona tu walimuweka chini ya ulinzi kwani alikuwa akisakwa
kwa udi na uvumba----wakati wa mahojiano alifichua siri na kueleza bayana
kusafirisha kilo 35 za mirungi” alisema Ndaki na kuongeza
“Polisi
walipoiona tu sura yake walimkwida na kumuweka chini ya ulinzi----nae hakufanya
shida kwani alikuwa akijua kuwa anawindwa na sasa anahojiwa kutoa taarifa ili
kuuzima mtandao wa usafirishaji mihadharati” alisema
Alisema
wakati polisi wakifichua mirungi hiyo ambayo ilikuwa imefichwa katika magunia
ya mkaa ilikuwa vigumu kuigundua lakini walipatwa na hofu baada ya kusikia
harufu kali iliyoasghiria mirungi.
Katika hali
nyengine, kaimu kamanda wa polisi aliwataka wananchi wanaoishi kandokando ya
milima ya Usambara Wilayani Korogwe na Lushoto kutoa taarifa za watu
wanaojishughulisha na kilimo cha bangi.
Alisema
kilimo hicho kimekuwa kikishamiri katika Wilaya hizo na hivyo kutoa wito kwa
wakulima waliobadilisha aina ya kilimo na badala yake kulima bangi kuwa msako
wa kuwasaka uko karibu.
“Natoa wito
kwa wakazi wanaoishi karibu na milima ambayo yunadhani kuna watu wamebadilisha
aina ya kilimo na kulima bangi kuwafichua na kutupa taarifa----polisi
imejipanga kufanya msako usiku na mchana” alisema Ndaki
Alisema
tabia ya watu kulima bangi badala kilimo cha chakula kunaifadhaisha jamii kwani
eneo hilo kila mwaka hukumbwa na njaa huku chanzo kikiwa ni wakulima
kubadilisha kilimo.
EmoticonEmoticon