Na: Atley Kuni- Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mh. Magesa Mulongo |
Wazee
katika Mkoa wa Mwanza, wamemshauri Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kuanza kulima
zao la alizeti ili kuuwezesha mkoa huo kuinuka kuichumi kutokana na
hali mbaya ya mazao kama pamba kupoteza umaarufu kwenye sekta ya uchumi
wa mkoa huo.
Wakizungumza
katika kikao kilicho wakutanisha wazee hao na mkuu wa mkoa hivi
karibuni katika hoteli ya Mwanza, wazee hao walisema kutokana na hali
isiyoridhisha kwa zao kama pamba ambalo ndilo lilikuwa zao kuu la uchumi
wa mkoa huu kupoteza umaarufu ni vema sasa jamii ikabadilika na
kuhamishia nguvu zake kwenye zao la alizeti.
Akizungumza
kwa niaba ya wazee wenzake, aliyekuwa Mkuu wa kwanza wa wilaya ya
Ilemela, Jared John Gachocha, alisema, haoni sababu ya mkoa wa Mwanza
kushindwa kutilia mkazo zao la alizeti ambalo gharama zake za uzalishaji
ni nafuu zaidi ukilinganisha na pamba.”
Mh.
Mkuu wa mkoa mimi nadhani kipindi hiki tushughulike kufa na kupona
kwenye alizeti, sioni kwa nini wenzetu wa Singida watupite katika hili,
zao la alizeti ni rahisi mno kulilima halina usumbufu halihitaji mbolea
nyingi, haliitaji maji mengi na maandalizi yake kwakweli ni rahisi
lakini pia faida yake ni kubwa” alisema na kuongeza kuwa “hali hiyo
itasaidia mkoa kujitosheleza kwa mafuta lakini pia kuweza kuuza kwa watu
wengine.
Mbali
ya zao la alizeti wazee hao pia walimuasa mkuu huyo wa mkoa, kuelekeza
nguvu zaidi kwenye masuala ya ufugaji, wakisema kuwa tupo nyuma sana
katika masuala ya mifugo huku wakitolea mfano nchi ya Kenya kwamba
Ng’ombe anauwezo wakutoa maziwa lita hadi 20 tofauti na Tanzania, hali
inayo walazimu wazee hao kumuasa mkuu wa mkoa kuwataka wafugaji kuachana
na ufugaji wa kizamani na badala yake watafute mitamba itakayoweza
kuleta tija kwa wafugaji. “Ni ukweli usiopingika kwamba hapa kwetu
kumpata ng’ombe anayeweza kukupatia lita 10 za maziwa ni nadra sana
hivyo tuwashawishi wakulima waweze kutafuta mitamba ambayo itakuwa niya
kisasa ili waweze kukuza uchumi wao lakini uchumi wa mkoa kwa ujumla.
Awali
akizungumza mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kabla yakuanza kupokea maoni ya
wazee hao, alisema mkoa wa Mwanza wenye watu Milioni mbili na laki saba
na mia saba sabini na mbili mia tano na tisa, huku mkoa ukiwa unachangia
Trioni 4.9 katika pato la taifa, Watu wake milioni moja uchumi wao
unategemea zaidi katika Sekta ya Uvuvi, “Wazee wangu nimewaiteni
tusaidiane kuongoza mkoa huu, mkoa huu ni mkubwa na changamoto tulizo
nazo ni nyingi” alisema Mulongo na kuongeza kuwa, “kati ya watu mil.
2.7, watu Milioni moja wanategemea ziwa kuanzia mvuvi ziwani hadi
mparuaji na mchuuzi mdogo mdogo wa mtaani sasa hali ya ziwa letu kwa
upande wa uzalishaji sio salama sana, tuna kwendaje lazima tujipange
kisawasawa alisema Mulongo.
Mkuu
wa mkoa wa Mwanza toka amewasili mkoa wa Mwanza, ameweka utaratibu
wakukutana na watu wa makundi mbali mbali mkoani hapa ili kufahamu
changamoto ambazo zipo ili waweze kuzitatua kwa kushirikiana kwa pamoja,
makundi ambayo tayari yamekutana na mkuu huyo wa mkoa hadi sasa ni
pamoja na, Wananchi wa kawaida kwa kuzungumza nao kwenye mikutano ya
hadhara na kusikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi, Wafanya biashara
wadogo ambao alifanikisha kufanyika kwa uchaguzi wao, wakuu wa taasisi
za umma zilizoko mkoani hapa, viongozi wa dini, viongozi wa kisiasa na
asasi zisizo za kiraiya.
Mkoa
wa Mwanza ni mkoa wa pili kwa uchangiaji wa pato la taifa kwa asilimia
9.15% ukitanguliwa na Mkoa wa Dar Es Salaam, huku wastani wa pato la
mwananchi wa kawaida ikiwa ni Tshs. 910,824 kwa mwaka.
EmoticonEmoticon