Beki wa Yanga, Edward Charles, ametupwa nje katika kikosi hicho kwa siku kumi, huku
mkongwe Kelvin Yondani akirejea
kuivaa BDF XI, siku ya Jumamosi katika raundi ya kwanza ya michuano ya Kombe la
Shirikisho.
Charles aliumia katika mchezo wao wa hivi
karibuni dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo aliumia kifundo cha mguu, akafungwa bandeji
nyepesi.
Yondani yeye aliumia kwenye mchezo kati ya
timu yake na Polisi Morogoro, lakini ameshapona na yupo fiti kwa mechi hiyo.
“Wachezaji wanaendelea vizuri kama hivi,
Yondani na Dilunga, wameanza mazoezi leo kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi baada
ya afya zao kuimarika lakini Edward yeye ataendelea kuwa nje kwa siku kumi
mpaka pale afya yake itakapoimarika.
“Upande wa beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’, yeye
leo (jana Jumanne), hajafanya mazoezi lakini kesho (leo) ndiyo ataanza rasmi na
timu kama kawaida, kwa sababu alipata maumivu kidogo katika mchezo wetu dhidi
ya Mtibwa Sugar na sasa yupo vizuri,” alisema Daktari wa Yanga, Sufiani Juma.
EmoticonEmoticon