Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam,
Ramadhani Madabida (katikati), akizungumza na makatibu waenezi 90 wa CCM
wakati akifungua semina elekezi ya siku moja kwa makatibu hao kutoka
Kata mbalimbali za mkoa wa Dar es Salaam leo. Kushoto ni Katibu Muenezi
wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba na Katibu Muenezi Msaidizi wa
CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Athuman Salum.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida (katikati), akizungumza na makatibu hao.
Makatibu Uenezi hao wakishangilia hutuba ya mgeni rasmi, Ramadhani Madabida.
Makatibu Uenezi kutoka Wilaya ya Kinondoni wakiwa kwenye semina hiyo.
Makatibu Uenezi kutoka Wilaya ya Temeke wakiwa kwenye semina hiyo.
Makatibu Uenezi kutoka Wilaya ya Ilala wakipitia taarifa yao ya utekelezaji wa Ilani ya CCM na uhai wa chama chao.
Makatibu uenezi wa Wilaya ya Ilala wakiwa kwenye semina hiyo.
Hapa makatibu hao wakiwa kwenye majadiliano.
Makatibu hao kutoka Wilaya ya Temeke wakifuatilia kwa makini hutuba ya mgeni Rasmi Ramadhani Madabida.
Makatibu uenezi hao wakiwa kwenye semina hiyo. Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Dotto Mwaibale
MWENYEKITI
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida
amewataka makatibu waenezi wa chama hicho kumtetea Rais Jakaya Kikwete
na chama hicho ili aendelee kuaminiwa na wananchi.
Madabida
alitoa mwito huo wakati akifungua semina elekezi ya siku moja
iliyoandaliwa mahususi kwa makatibu waenezi 90 wa chama hicho kutoka
kata mbalimbali za mkoa wa Dar es Salaam iliyofanyika leo ofisi ya CCM
Wilaya ya Ilala.
“Ninyi ni
kama maofisa mawasiliano na masoko hivyo mnawajibu wa kukiuza na
kukitangaza chama chetu kwa wananchi ili waendelee kuwa na imani nacho
na serikali kwa ujumla” alisema Madabida.
Alisema
kazi yenu kubwa ni kumtetea rais ambaye ni Mwenyekiti wetu wa chama
taifa na ili aendelee kuheshimika kwa wananchi hasa pale anapochafuliwa
na wapinzani.
Katika
hatua nyingine Madabida aliwataka makatibu ueneze hao kuwa wamoja na
kuacha kuwachukia viongozi waliopo madaraka baada ya chaguzi kuisha na
akatoa onyo kuwa hata kuwa na mswalia mtume kwa mtu atakayebainika
kuendeleza chuki hicho.
“Kumekuwa
na tabia ya watu kuendeleza chuki baada ya kukosa nafasi katika
uchaguzi hivyo kutufanya tushindwe kusonga mbele nasema katika hilo
mtaniita majina mengi mabaya kwani siqwezi kumvumilia mtu” aliongeza
Madabida.
Madabida
aliwataka makatibu uenezi hao kufanya mikutano ya hadhara ili kukinadi
chama chao kwani wenye wajibu wa kutekeleza ilani ya chama ni wao na si
mtu mwingine.
EmoticonEmoticon