Rama ametua kwenye klabu ya Coastal Union akitokea nchini Kenya na kusaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Rama aliyewahi kuicheza timu hiyo kwa mafanikio makubwa na kufanikiwa kupata namba kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Kenya Harembee Stars alitua jijini Tanga juzi usiku akiwa na kulakiwa na viongozi wa klabu hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye makao makuu ya Klabu hiyo barabara 11,Katibu wa Coastal Union,Kassim El Siagi amesema kikosi cha cha timu hiyo msimu ujao kinatarajiwa kuwa tishio kutokana na kufanya usajili wa nguvu ambao unaonekana utaleta upinzani mkubwa sana.
Aidha amesema kikosi chetu msimu ujao kitakuwa tishio kwa
sababu tunamatumaini makubwa ya kufanya vizuri kutokana na usajili imara ambao tumeufanya kwa kusajlili wachezaji nyota kama vile Obina,Shabani Kado Sued Tumba ,Bakari Mtama, na wengine wengi walipo kwenye kikosi cha timu hiyo
Amesema bado wanaendelea na mchakato wa kuhakikisha wanaimarisha kikosi hicho kwa ajili ya maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa ligikuu Tanzania bara msimu ujao.
EmoticonEmoticon