WAGOSI WA KAYA COASTAL UNION KUTUA PEMBA JUMANNE

August 17, 2014

Na Mwandishi Wetu, Tanga

TIMU ya Coastal Union ya Tanga inatarajiwa kundoka mkoani hapa Jumanne kuelekea Kisiwani Pemba kwa ajili ya kuweka kambi ya Mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi kuu soka Tanzania bara.
 Akizungumza wa waandishi wa habari leo katibu Mkuu wa Coastal Union,Kassim El Siagi amesema kuwa kambi hiyo itawekwa visiwani humo pamoja na kufanyia mazoezi kwenye uwanja wa Migombani kila siku.
 El Siagi amesema kuwa kikosi cha wachezaji wapatao 25 ikiwemo Benchi la Ufundi litakuwa na watu watano ambao wataelekea visiwani humo wakiwa na lengo la kukisuka kikosi hicho kwa ajili ya kuleta ushindani msimu ujao.
 Amesema katika benchi la ufundi litakuwa na Kocha mkuu Yusuph Chipoo,Kocha Msaidizi Benard Mwalala na Kocha wa makipa Razack Siwa,Daktari wa timu pamaoja na Kiti meneja.
 
 
 Aidha amesema msafara wa timu hiyo utaondoka mapema mkoani hapa siku hiyo kwa ajili ya kwenda kuanza kambi mpya ya maandalizi ya kuelekea msimu mpya wa Ligi kuu Tanzania bara.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »