Na Elias Kimaro
MREMBO wa Kanda ya
Ziwa 2014, ‘Miss Lake Zone 2014’, anataibuka na zawadi ya gari aina ya Vitz
lenye thamani ya Sh.10,000,000, katika shindano litakalofanyika Agosti 30 CCM
Kirumba.
Akizungumza na TANGA RAHA BLOG,
muandaaji wa shindano hilo, Flora Lauwo, alisema jumla ya warembo 18
wanatarajiwa kuchuana kuwania zawadi hiyo iliyotolewa na Lenny wa Geita.
“Shindano hili
limedhaminiwa na kampuni ya bia TBL kupitia kinywaji cha Redd’s na
Pepsi…shindano hili litafanyika Kirumba baada ya lile la Miss Talent kufanyika
Agosti 23 mkoani Geita,” alisema Lauwo.
Aidha, Lauwo alisema
washindi watano wa awali watapewa ving’amuzi, na mshindi wa tatu wa Miss talent
atapata Bajaj yenye thamani ya Sh.3,000,000.
Awali, meneja wa
matukio wa TBL kanda ya ziwa, Erick Mwayela, alisema kampuni yake imekuwa
mstari wa mble kudhamini vipaji vya warembo kwa miaka mingi.
“Lengo la kampuni
yetu ni kuendeleza vipaji vya warembo na mavazi nchini,” alisema Mwayela.
Warembo watakaowania
zawadi hiyo ya kwanza ni Christina William, Moshi Shaban na Doreen Robert wote
wa Mwanza, Cecilia Kibanda, Evelyne Charles, Chritine John (Simiyu), Winfrida
Nashon, Elinaja Nnko na Martha John wote toka Mara.
Wengine ni Mary
Emanuel, Nicole Sarakyika na Recho Judica toka Shinyanga, Jackline Kimanbo, Nyangi
Warioba na Faudhia Haruna (Kagera), wakati toka Geita ni Recho Clavery, Farida
Ramadhani na Rose Msuya.
EmoticonEmoticon