ABSAM MABINGWA WA POOL TABLE TANGA.

August 17, 2014
NA MWANDISHI WETU,TANGA.
CLUB ya Absam Pool mwishoni mwa wiki walitawazwa kuwa mabingwa wapya wa mchezo wa Pool Table ngazi ya Mkoa wa Tanga na kukabidhiwa kitita cha sh.800, 000 baada ya kuibuka kidede kwenye mchezo wa fainali dhidi yao na Young Boys.

Fainali hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Fax Night Club uliopo jijini Tanga ilikuwa na upinzani mkubwa kutokana na timu hizo wachezaji wa timu zilizokuwa zikishiriki kuchukua vikali.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na Club ya Young Boys ambao walizawadiwa kitita cha sh.400,000 wakati mshindi wa tatu Spider walikabidhiwa kitita cha sh.250,000 huku mshindi wanne Kange Brothers wakizawadiwa kitita cha 150,000 na mgeni rasmi kwenye mashindano hayo Ofisa Utamaduni wa Jiji la Tanga Peter Semfuko.

Katika mshindi mmoja mmoja kwa upande wa wanaume, Abeid Juma kutoka Club ya Spider aliweza kuibuka kidedea na kufanikiwa kuondoka na kitita cha sh.400, 000 kwa kumshinda Ajinabi Baruti kwenye mchezo wa Fainali.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na Ajinabi Baruti aliyazawadiwa 250,000, Nafasi ya tatu ikichukuliwa na Iddi Abasi Karonga ambaye alizawadiwa kitita cha sh.250,000 wakata nafasi ya nne ilichukuliwa na Tifu Abdallah aliyepata 100,000

Kwa upande wa wanawake bingwa alikuwa ni Neema Hamisi baada ya kumbwaga mpinzani wake Zainabu Kishingo kwenye mchezo wa fainali na kupata kitita cha sh.300,000,mshindi wa pili Zainabu Kishindo akizawadiwa 200,000,mshindi wa tatu alikuwa ni Halima Hamisi ambaye aliondoka na kitita cha sh.100,000 na nafasi ya nne ilichukuliwa na Mariam Raphael aliyejipatia 50,000

Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao, Semfuko ambaye alikuwa mgeni rasmi aliwataka wachezaji wa mchezo wa Pool Table mkoani Tanga kuhakikisha wanauthamini mchezo huo ili waweza kupata fursa mbalimbali zinazotokana nazo lengo likiwa kujikwamua kiuchumi na maisha

Alisema wakitumia kucheza mchezo huo unaweza kuwaepusha kukaa vijiweni ambapo hutumia muda mwingi kufikiria matumizi ya madawa ya kulevya.

Hata hiyo Ofisa Utamaduni huyo aliwataka kuacha kucheza kiholela holela badala yake wafuate taratibu zilizopo ikiwemo kuvisajili vilabu vyao ili viweze kutambulika.

   “Michezo ni ajira ambayo inaweza kuwainua kimaisha hivyo nawasihi mzingatie michezo hasa mchezo wa Pool table kwani unaweza kuwainua kimaisha kama mtautilia mkazo “Alisema Ofisa Utamaduni Semfuko.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »