Leo majira ya saa nne na nusu Asubuhi ndani ya Mkoa wa
Kilimanjaro mashabiki mbalimbali wa Mpira wa miguu hususani Mashabiki na wanazi
wa Timu kongwe ya mpira wa Miguu Daresalaam Yanga African Walikua katika
barabara kuu ya Moshi Arusha kuipokea Timu ya Yanga.
Basi la Yanga likiwa nje ya kituo cha Mafuta cha Panone kilichopo weruweru nje kidogo ya Mji wa Moshi.
Timu ya Yanga ambayo inatarajia kushuka dimbani hapo kesho
katika Mechi ya kirafiki dhidi ya Timu ya Panone Fc ambayo ni Mabingwa wa Ligi Daraja la Tatu mkoa
Kilimanjaro. Mchezo huo uliodhaminiwa na Panone and Co. Ltd na Ngiloi ulomi
enterprises huku wakishirikiana na wadau mbalimbali wa mpira wa Miguu mkoani
Kilimanjaro ambao ni Ngorika bus Service, Kili Fm Radio, Kifaru oil, Malindi
Night Club, Ibra Line, Marenga Investment co. Ltd na Moshi fm Radio. Katika kufanikisha hilo
Panone wamejiandaa kuhakikisha Historia ya Kimichezo inavunjwa kwani Yanga
imewahi kucheza ndani ya Kilimanjaro Miaka 23 iliyopita.
Mchezaji wa Yanga Didie Kavumbagu akifurahia Mandhari ya Mji wa Moshi.
Tukizungumza na Kocha mkuu wa yanga Hans Plujim kuhusiana na mchezo huo baada
ya kuwasili Moshi mkoani Kilimanjaro. Amesema anategemea kutumia Mchezo huo wa
Kirafiki na Timu ya Panone Fc kama mchezo wa Maandalizi wa mechi yao ya mwisho
dhidi ya timu ya Simba Sport Club. Akizungumzia kikosi atakachokichezesha
amesema anategemea kuchezesha wachezaji ambao watacheza na yanga ndio maana
amebeba wachezaji 21 kwa ajili ya mchezo huu.
Meneja wa Panone and Co. Ltd Gido Marandu akiwa na Kocha Mkuu wa Yanga Hans Plujim na Kocha Msaidizi ndugu Mkwasa Baada ya Kuwapokea Katika Kituo cha Mafuta Cha Panone Kilichopo Weruweru leo Asubuhi.
Akizungumza nasi Meneja wa Panone and Co. Ltd kwa kanda ya
Kaskazini ndugu Gido marandu amesema Kampuni imejiandaa vizuri kuweza
kuhakikisha kilakitu kinakwenda sawa na Timu ya Yanga imeshawasili. Hata hivyo
alitaja Viingilio nitakua shilingi 10000 kwa viti maalumu na 7000 kwa viti
maalumu B na shilingi 5000 kwa Mzunguko. Kuhusu suala la Ulinzi alisema ulinzi
uko wa Kutosha kutoka kwa Jeshi la Polisi na Kampuni ya ulinzi wenye Dhamana ya
kuhakikisha ulinzi unakua hapo.
Alimaliza kwa kusema “Huu ni wasaa wa washabiki na wapenzi wa
timu ya Yanga ndani ya mkoa wa kilimanjaro baada ya miaka mingi kukosa mchezo
mkubwa ndani ya mkoa wetu na huu ndio mwanzo tu”
Mchezaji wa Yanga Mrisho Ngasa Akiwa ametulia katika Gari baada ya Kuwasili Moshi.
EmoticonEmoticon