Wachezaji
wa Azam Fc, wakishangilia ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya city
katika mchezo wao wa Ligi Kuu uliochezwa jana Jijini Mbeya na kutangaza
ubingwa rasmi kwa kufikisha jumla ya Pointi 59 wakiwaacha Yanga ambao
nao pia waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Orjolo walicheza
jana jijini Arusha na kufikisha jumla ya Pointi 55 huku wakiwa wamesalia
na mchezo mmoja dhidi yao na Simba utakaochezwa Aprili 19, ambao hata
wakishinda hawataweza kufikia pointi za wapinzani wao katika mbio hizo
Azam, ambao nao pia wamesalia na mchezo mmoja ambao hata wakishinda au
kushinda hauna faida wala hasara kwao.
BAADA ya Azam
kufanikiwa kutwaa taji la ubingwa jana jijini Mbeya kwa kuwalaza wenyeji
wao Mbeya City, imeweka rekodi ya kuwa klabu ya tisa kunyakua taji hilo nchini
tangu mwaka 1965.
Azam imetwaa ubingwa huo ikiwa na
jumla ya Pointi 59 ikiwa imecheza michezo
25, huku wapinzani wao katika mbio hizo, Yanga wakibaki nafasi ya pili
baada kuwabamiza Oljoro JKT mabao 2-1 katika mchezo wao uliopigwa kwenye
Uwanja wa Sheikh AMri Abeid jijini Arusha na kufikisha jumla ya Pointi
55.
Azam waliweza kushika nafasi ya pili
misimu miwili
mfululizo nyuma ya Simba na Yanga, ambapo msimu huu wameonyesha uchu wa
kuitamani na kumudu kuiwania vyema nafasi ya kwanza na hatimaye
kufanikiwa.
Ukiondoa Yanga na Simba walionyakua mataji
mara nyingi, Azam itaingia kwenye orodha ya walionyakua ubingwa huo ikifuata
nyayo za Cosmopolitan iliyofanya hivyo kwa mara ya kwanza mwaka 1967.
Baada ya Cosmo waliofuata walikuwa ni Mseto ya Morogoro
waliofanya hivyo mwaka 1975, kisha Pan Africans iliyoweka rekodi mwaka 1982,
ikafuatiwa na Tukuyu Stars iliyonyakua mwaka 1986 na kufuatiwa na Wagosi wa Kaya,
Coastal Union mwaka 1988.
Klabu ya Mtibwa Sugar ilikuja kuweka rekodi ya
kunyakua taji hilo la Ligi Kuu misimu miwili mfululizo mwaka 1999 na 2000 kabla
ya Simba na Yanga kupokezana taji hilo tangu hapo hadi msimu huu ambapo
inaelekea wazi Azam wanaingia kwenye orodha hiyo.
Azam imeweka rekodi hiyo ya kuwa timu ya tisa kunyakua taji hilo na
kuisimamisha Yanga iliyoshikilia taji hilo la 24, ikiongoza
orodha ya klabu zilizonyakua mara nyingi ikifuatiwa na Simba iliyotwaa mara 18.
ORODHA KAMILI YA MABINGWA WA LIGI KUU TANGU 1965-
1965 Sunderland (Simba)
1966 Sunderland
1967 Cosmopolitan
1968 Yanga
1969 Yanga
1970 Yanga
1971 Yanga
1972 Yanga
1973 Simba
1974 Yanga
1975 Mseto
1976 Simba
1977 Simba
1978 Simba
1979 Simba
1980 Simba
1981 Yanga
1982 Pan Africans
1983 Yanga
1984 Simba
1985 Yanga
1986 Tukuyu Stars
1987 Yanga
1988 Coastal Union
1989 Yanga
1990 Simba
1991 Yanga
1992 Yanga
1993 Yanga
1994 Simba
1995 Simba
1996 Yanga
1997 Yanga
1998 Yanga
1999 Mtibwa Sugar
2000 Mtibwa Sugar
2001 Simba
2002 Yanga
2003 Simba
2004 Simba
2005 Yanga
2006 Yanga
2007 Simba
2007/08 Yanga
2000-09 Yanga
2009-10 Simba SC
2010-11 Yanga
2011-12 Simba SC
2012-13 Yanga
2013-14 Azam Fc
EmoticonEmoticon