Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Jerome Valcke
atawasili nchini Mei 1 mwaka huu ambapo atafungua semina ya mawasiliano
itakayoshirikisha viongozi wa vyama wanachama wa Baraza la Vyama vya
Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Akizungumza
Dar es Salaam leo (Aprili 14 mwaka huu), Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema Valcke ambaye hii ni mara
yake ya kwanza kuja Tanzania atafuatana na maofisa wengine wa saba wa
FIFA.
Amesema
semina hiyo iliyoandaliwa na FIFA itafanyika kwa siku mbili (Mei 1 na 2
mwaka huu) ambapo vilevile Valcke atapata fursa ya kuzungumza na
waandishi wa habari wa ndani na wa kimataifa.
Rais
Malinzi amesema washiriki wa semina hiyo ni marais, makatibu wakuu na
wakuu wa mawasiliano wa wanachama 12 wa CECAFA ambao ni Burundi,
Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Somali, Sudan, Sudan Kusini,
Tanzania na Uganda.
Naye
Mwenyekiti wa CECAFA, Leodegar Tenga ambaye alifuatana na Katibu Mkuu
wake Nicholas Musonye amemshukuru Rais wa TFF kwa kukubali kuwa mwenyeji
wa semina hiyo kwani itasaidia katika maendeleo ya mpira wa miguu
katika ukanda huu.
EmoticonEmoticon