Miss
Ilala 2013, Doris Mollel ijumaa ya wiki iliyopita alitembelea shule ya
msingi Pugu jijini Dar es Salaam na kukabidhi vitabu 50 za hadithi kwa
wanafunzi wa shule hiyo katika harakati zake binafsi za kuwajengea
wanafunzi na watoto utamaduni na tabia ya kujisomea kwenye umri mdogo.
Miss Ilala huyo wa mwaka 2013 alitumia nafasi hiyo kuwahamasisha wanafunzi kujisomea kama ufunguo wa maisha yao ya baadaye.
Miss
Ilala 2013, Doris Mollel akimkabidhi vitabu Mwalimu Josephine Matiku
kwenye hafla rasmi ya makabidhiano shule hapo ijumaa iliyopita jijini
Dar.
Miss Ilala 2013, Doris Mollel akipozi na walimu wa shule hiyo wakati wa halfa ya kukabidhi vitabu.
Miss Ilala 2013, Doris Mollel katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Pugu.
EmoticonEmoticon