Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na
Michezo ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Michezo na
Burudani kuelekea maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Bw.
Leonard Thadeo wakwanza kulia akiongoza tamasha la mazoezi ya viungo
kwa Watumishi wa Serikali na Mashirika ya Umma mapema wikiendi hii
katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,Tamasha hilo ni muendelezo
wa program mbalimbali za kuadhimisha Muungano kwa njia ya Mchezo na
Burudani.
Baadhi
ya watumishi wa Serikali na Mashirika ya Umma wakiwa katika tamasha la
michezo katika kuadhimisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mapema
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali Watu wa wizara ya Habara, Vijana, Utamaduni na
Michezo Bw. Barnabas Ndunguru(kushoto) na Afisa Tawala wa Wizara hiyo
Bw. Mussa Varisanga wakifanya mazoezi wakatio wqa Tamasha la mchezo kwa
ajili ya kuadhimisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika
mapema mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mtumishi
kutoka Wizara ya Ulinzi Bw. Abdul Nyumba akiwaongoza watumishi wenzake
katika mazoezi ya viungo mapema mwishoni mwa wiki wakati wa Tamasha la
Michezo kwa ajili ya maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na
Michezo ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Michezo na
Burudani kuelekea maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Bw.
Leonard Thadeo akizungumza na watumishi kutoka wizara mbalimbali na
mashirika ya Umma walioshiki tamasha la michezo kwa ajili ya kuadhimisha
Muungano mapema wikiendi hii. Picha na Frank Shija.
EmoticonEmoticon