Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikaribishwa na viongozi wa
jeshi wakati alipokwenda kukabidhi Mabasi 10 chakavu ya Vyombo vya
Ulinzi na Usalama kwa kampuni ya Dar Coach kwa ajili kufufuliwa upya na
kuwa ya kisasa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amekabidhi Mabasi 10
chakavu ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kampuni ya Dar Coach kwa
ajili kufufuliwa upya na kuwa ya kisasa.
Mabasi hayo 10 chakavu yanatoka kwenye Vyombo vya Ulinzi na Usalama
ikiwemo Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Magari 3, Jeshi la Polisi
Magari 4 pamoja na Jeshi la Magereza Magari 3 ambapo yote kwa pamoja
Matengenezo yake yameokoa kiasi cha Shilingi Billion 1,110,000,000 ya
Serikali.
Makonda amesema kuwa Gari hizo zitatengenezwa na kukamilika ndani ya
Siku 90 hadi 120 ambapo ameipongeza Kampuni ya Dar Coach kwa kujitolea
kukarabati Magari hayo bila kutumia pesa ya Serikali.
Aidha Makonda amesema Magari hayo yatafungwa Vifaa vya Kisasa ikiwemo
Kiyoyozi (AC), Mfumo wa Chaji ya Simu kila Seat, Runinga, Radio, Viti
vya kisasa, Vyoo vya Ndani, Bodi mpya pamoja na mwonekano mzima wa Gari
ili ziwe za kisasa.
Amesema mpango wake wa kuendelea kuongezea nguvu Vyombo vya Ulinzi na
Usalama hautokoma kwakuwa lengo lake ni kuwatumikia Wananchi na Askari
wajivunie kufanyakazi chini ya Mkuu wa Mkoa mwenye kuwapenda na
kuwajali.
Amemuagiza Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Lazaro
Mambosasa kuhakikisha Ving'ora vya Jeshi la Polisi vinakuwa tofauti na
kampuni za Ulinzi na Usalama, Magari ya Wagonjwa ili kupunguza
Mkanganyiko kwa wananchi na kujengea heshima Jeshi la Polisi.
Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na
usalama akiwemo Kamanda wa Polisi Dar es Salaam Lazaro Mambosasa,
Mkurugenzi wa usafirishaji JWTZ Kanal RAajab Mwenyumbu, Mnadhimu wa
Jeshi la Magereza ACP. Noel James ambapo wote kwa pamoja wamempongeza
mkuu wa mkoa kwa hatua kubwa anayoifanya ya kuhakikisha wanafanya kazi
katika mazingira mazuri.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akimkabidhi Mabasi 10
chakavu ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Dar
Coach kwa ajili kufufuliwa upya na kuwa ya kisasa wakishuhudiwa na Mkuu
wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaviva,Kamanda wa Polisi Dar es Salaam
Lazaro Mambosasa, Mkurugenzi wa usafirishaji JWTZ Kanal RAajab
Mwenyumbu, Mnadhimu wa Jeshi la Magereza ACP. Noel James.
Mabasi 10 chakavu yakiwa yanatoka katika Chuo cha Polisi Kilwa Road
kuelekea Mkuranga kwenye ofisi za Kampuni ya Dar Coach kwa ajili ya
kufanyiwa marekebisho na kuwa ya kisasa zaidi.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa sambamba na Mkuu wa Wilaya
ya Temeke Felix Lyaviva,Kamanda wa Polisi Dar es Salaam Lazaro
Mambosasa, Mkurugenzi wa usafirishaji JWTZ Kanal RAajab Mwenyumbu,
Mnadhimu wa Jeshi la Magereza ACP. Noel James wakati wa kukagua mabasi
10 chakavu kabla ya kupelekewa kwenye gereji ya Dar Coach kwa ajili ya
matengenezo.Picha zote na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
EmoticonEmoticon