Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh. Anthony Mavunde akizungumza na
vijana katika Chuo cha Ufundi Don Bosco kilichopo mkoani Kilimanjaro
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh. Anthony Mavunde akikagua maendeleo
ya Vijana ambao wanasomeshwa na Serikali kupitia mpango wa Ukuzaji
Ujuzi Nchini katika Chuo cha Ufundi Don Bosco kilichopo mkoani
Kilimanjaro.
…………….
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh. Anthony Mavunde leo ametembelea
Chuo cha Ufundi Don Bosco kilichopo mkoani Kilimanjaro na kukagua
maendeleo ya Vijana ambao wanasomeshwa hapo na Serikali kupitia mpango
wa Ukuzaji Ujuzi Nchini.
Akizungumza na Vijana hao ambao
wanasomea masomo ya Komputa,Mavunde amewataka Vijana hao kuutumia ujuzi
watakaoupata hapo chuoni kujiajiri kwa kuunda vikundi na Makampuni ili
wapate nafasi ya kuwezeshwa kupitia mifuko ya uwezeshwaji wananchi
kiuchumi nchini na hivyo kusaidia kutatua changamoto ya ukosefu wa Ajira
kwa Vijana.
Mavunde pia amewaeleza Vijana hao
kwamba watambue siku zote wao ndio moyo wa Taifa na hivyo ndio nguvu
kazi inayotegemewa kwa kiasi kikubwa ndio maana Serikali inaona umuhimu
wa kuwekeza katika Mpango huu wa ukuzaji Ujuzi ili kuhakikisha Taifa
linakuwa na nguvu kazi yenye ujuzi stahiki katika kuelekea nchi Uchumi
wa Viwanda na ya kipato cha kati.
Kwa upande wao Vijana hao
wanufaika na Mpango huu wameishukuru serikali kwa kutekeleza mpango huu
wa ukuzaji ujuzi ambao utawasaidia kupata ujuzi na baadaye kuweza
kujiajiri na Kuajiri Vijana wengine.
Mpango huu wa ukuzaji ujuzi
unatarajia kuwanufaisha Vijana 3445 ambao serikali itagharamia mafunzo
yao katika kozi za Tehama,Umeme,Ushonaji,Useremala,Uchomeleaji,Kuweka
vigae,Ufundi bomba,Upigaji chapa na Ufundi Magari.
EmoticonEmoticon