Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (mbele),
akitoka kuangalia ukarabati wa meli ya Mv. Clarius, katika Bandari ya
Mwanza, leo. Meli hiyo inatoa huduma katika visiwa vilivyo kwenye ziwa
Victoria.
Muonekano
wa Meli ya Mv. Umoja yenye uwezo wa kubeba behewa 22. Meli hiyo
inasafirisha mizigo kutoka Bandari ya Mwanza kuelekea Bandari ya “Port
Bell” Uganda.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa nne
kulia), akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli
(MSCL), Xavier Kapinga, alipofika Bandari ya Mwanza leo kujionea
maendeleo ya ukarabati wa meli ya MV. Clarias katika Bandari hiyo.
Mhandisi
Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Xavier Kapinga, akifafanua
jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame
Mbarawa (Wa tatu kushoto mbele) wakati alipokagua maendeleo ya ukarabati
wa meli katika Bandari ya Mwanza, leo.
Meneja
Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Bw. Erick Hamissi,
akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame
Mbarawa (Wa pili kulia), hatua zilizofikiwa za ukarabati wa meli ya Mv.
Clarius na Mv. Umoja katika Bandari ya Mwanza.
Mafundi
wakiendelea na ukarabati wa meli ya Mv. Clarius leo katika Bandari ya
Mwanza. Kukamilika kwa ukarabati wa Meli hiyo inayotoa huduma katika
visiwa vilivyo katika ziwa Victoria kutarudisha huduma za usafirishaji
na abiria katika visiwa hivyo.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amekagua
eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya na yakisasa
itakayotoa huduma za usafirishaji katika Ziwa Victoria.
Akizungumza
na wafanyakazi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Profesa Mbarawa,
amewataka wafanyakazi wa Kampuni hiyo kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi
ili kazi hiyo ianze mara moja na kukamilika kwa wakati.
“Mkandarasi
ameshapatikana hivyo hakikisheni mnatoa ushirikiano na mnafanya uhakiki
wa kimahesabu vizuri ili kazi hii ifanyike kwa gharama nafuu, ubora na
muda mfupi”, amesema Profesa Mbarawa.Katika
hatua nyingine, Waziri Mbarawa, amekagua maendeleo ya ukarabati wa meli
ya Mv. Clarias na Mv. Umoja ambapo ameeleza kuridhishwa kwake na hatua
zilizofikiwa, na hivyo kuwataka MSCL kutafuta mizigo ya kusafirisha
kutoka Bandari ya Mwanza kwenda Bandari ya “Port Bell”, nchini Uganda.
“Kukamilika
kwa meli kuwiane na kasi ya kutafuta mzigo mwingi ili meli hizi zifanye
biashara wakati wote na kuhakikisha Kampuni yenu inapata mapato mengi
yatakayowawezesha kujiendesha kwa faida”, amesisitiza Waziri Mbarawa.
Naye,
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Bw. Erick Hamissi,
amemhakikishia Profesa Mbarawa, kuwa wamejipanga kufanya ukarabati
mkubwa wa meli za Mv. Victoria, Butiama na Liemba ili kuziwezesha meli
hizo kufanya kazi katika ubora wake wa awali na kupunguza tatizo la
usafiri katika ziwa Victoria na Tanganyika.
“Tumeweka
mkakati wa kuhakikisha tunazikarabati meli zetu zote ili ziwe katika
ubora unaostahili wakati wote”, amefafanua Bw. Hamissi.
Katika
kuhakikisha maendeleo ya kibiashara na kuichumi yanafikiwa katika
Ukanda wa maziwa makuu nchini, Serikali imejipanga kuhakikisha inafufua
usafiri wa meli za abiri na mizigo katika ukanda huo.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
EmoticonEmoticon