Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joackim Wangabo amewatahadharisha watumishi
kutobweteka baada ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu
Zelote Stephen kustaafu na kumkabidhi yeye kijiti cha utekelezaji wa
shughuli za maendeleo ya mkoa.
Amesema
kuwa hatomwangusha Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kumuamini na
kumkabidhi madaraka hayo na kuahidi kuwa ataimarisha elimu inayoonekana
bado ipo chini kwa ufaulu lakini pia kuendeleza kasi ya uzalishaji
katika kilimo.
“Baada
ya kusoma kabrasha hili la kukabidhiana ofisi kuna mambo mengi ya
kuyazingatia ikiwemo, elimu, kilimo, ulinzi na usalama, utunzaji wa
mazingira, uvuvi na uwekezaji katika viwanda. Hasa katika elimu maana
mimba ni nyingi, kuna upungufu wa madawati, upungufu wa vyumba vya
madarasa lakini pia kiwango cha ufaulu hakijafikia kile kilichopo katika
ilani ya Chama cha Mapinduzi ambayo ni asilimia 80 kwa darasa la saba,”
Alisisitiza.
Mh.
Wangabo ameyasema hayo katika makabidhiano ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa mapema leo hii tarehe 31/10/2017 katika ukumbi wa ofisi hiyo,
jambo lililoshuhudiwa na watumishi wa sekretariet ya Mkoa pamoja na
baadha ya Halamashauri.
Katika
kuhakikisha utendaji kazi unakuwa wa ufanisi Mh. Wangabo amesema kuwa
hupemda kusikiliza mipango ya watendaji inayotekelezeka ili waweze
kuitekeleza kama walivyoipanga nay eye ataisimamia na kutoa ushauri wa
kuongeza kasi ya utekelezaji pale inapobidi ili kuyafikia malengo
waliyojiwekea kwa wakati.
Kwa
upande wake aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote
Stephen amewashukuru watumishi wote wa serikali katika Mkoa wa Rukwa
pamoja na wananchi wa mkoa kwa kumpa ushirikiano katika kipindi chote
alichokuwepo na kuwaomba waendeleze kumpa ushirikiano huo huo Mkuu wa
Mkoa mpya ili naye aweze kufanya majukumu yake kwa ufanisi.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joackim Leonard Wangabo (kushoto) na Mh. Zelote
Stephen (Waliokaa) katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama
ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri
na Mwenyekiti wa CCM Mkoa.
Mkuu
nwa Mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Leonard Wangabo akisalimiana na Meneja
wa PS3 Mkoa wa Rukwa Bi. Rose wakati wa kumkaribisha Mh. Wangabo katika
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa tayari kwaajili ya Kuanza kazi.
Aliyekuwa
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (kushoto)
akimkabidhi nyaraka za ofisi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joackim Wangabo.
katika makabidhiano ya ofisi hiyo yaliyofanyika katika ukumbi wa ofisi
ya Mkuu wa Mkoa.
Aliyekuwa
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (kushoto)
akisaini nyaraka za ofisi Mkuu wa Mkoa kwaajili ya Kumkabidhi ofisi hiyo
Rukwa Mh. Joackim Wangabo.
EmoticonEmoticon