Kuna Akaunti mpya wa Twitter inazunguka katika mitandao ya kijamii.
Akaunti hiyo yenye jina la Rais wa Shirikisho l Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), imeanza kutoa taarifa mbalimbali na kuchangia maoni
kunakoelezwa kufanywa na Wallace Karia.
TFF tunatangaza kuwa hatuitambui akaunti hiyo. Rais Karia hajafungua akaunti ya Twitter.
Tunaomba wananchi wote hususani wanafamilia wa mpira wa miguu,
kutoitambua akaunti hiyo kwa sababu si ridhaa ya Rais Karia wala Kitengo
cha Habari TFF kilichofungua akaunti hiyo.
EmoticonEmoticon