Rais wa Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli ameanza rasmi ziara ya kikazi ya
siku mbili nchini Rwanda ambapo amepokelewa na mwenyeji wake Rais Mh.
Paul Kagame wa Rwanda kwenye mpaka wa Rusumo ambapo viongozi hao wote
kwa pamoja wamefanya tukio la Kuzindua daraja la Lusumo linalounganisha
nchi za Rwanda na Tanzania na pia wamezindua kituo cha Forodha kilichopo
upande wa Rwanda katika mpaka huo, kama wanavyoonekana wakikata Utepe
kuashiria uzinduzi rasmi wa daraja la Lusumo watatu kulia katika picha
ni Mwakilishi wa benki ya ADB Dkt. Tonia Kandiero,
kutoka kulia ni Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshiba na
Waziri wa Ujenzi Tanzania Mh. Profesa Makame Mbarawa
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli na mwenyeji wake Rais Mh. Paul
Kagame wa Rwanda pamoja na viongozi wengine walioshiriki katika uzinduzi
huo wakipiga makofi mara baada ya kulizindua rasmi, watatu kulia katika
picha ni mwakilishi wa benki ya ADB Dkt. Tonia
Kandiero, kutoka kulia ni Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu
Yoshiba na Waziri wa Ujenzi Tanzania Mh. Profesa Makame Mbarawa
Daraja la Lusumo linalounganisha nchi za Tanzania na Rwanda linavyoonekana mara baada ya kuzinduliwa na marais hao leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli na mwenyeji wake Rais Mh. Paul
Kagame wa Rwanda pamoja na viongozi wengine wakikata utepe kuashiria
uzinduzi wa kiuo cha Forodha katika mpaka wa Rwanda na Tanzania uliopo
Lusumo katika picha kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mh. Agustine Mahiga
na Mwakilishi wa benki ya ADB Dkt. Tonia Kandiero pamoja na balozi wa Japan na viongozi mbalimbali waliohudhuria katika uzinduzi huo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania Mh. Dk. John Pombe Magufuli na mwenyeji wake Rais Mh. Paul
Kagame wa Rwanda pamoja na wake zao Mama Janet Magufuli na Mama
Jeannette Kagame mabalozi, Mawaziri wa nchi hizi mbili pamoja na
viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi
wa kituo cha Forodha kilichopo Lusumo mpakani mwa Tanzania na Rwanda
Jiwe lenye kibao linaloelezea uzinduzi huo na lenye majina ya viongozi wa nchi hizo mbili za Rwanda na Tanzania.
EmoticonEmoticon