Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Mhandisi John William Kijazi akifungua mafunzo ya Wakuu wa Mashirika na
Taasisi za Umma yalioandaliwa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili
ya Viongozi wa Umma leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Kamishna wa
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda.
Kamishna wa Sekretarieti ya
Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda akitoa maelezo
mafupi yanayohusu Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa
Umma wakati wa mafunzo ya Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma leo
jijini Dar es salaam. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John
William Kijazi.
Baadhi ya Washiriki wa mafunzo ya
Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma waliohudhuria mafunzo ya maadili
yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa
Umma leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Washiriki wa mafunzo ya
Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma waliohudhuria mafunzo ya maadili
yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa
Umma wakimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John William
Kijazi (hayupo pichani) leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Washiriki wa mafunzo ya
Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma waliohudhuria mafunzo ya maadili
yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa
Umma wakimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John William
Kijazi leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Mhandisi John William Kijazi akiongea na Waandishi wa habari mara baada
ya kufungua mafunzo ya Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma
yalioandaliwa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa
Umma leo jijini Dar es salaam.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
…………………………………………………………………………………………………………….
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Mhandisi John William Kijazi amewaasa Wakuu wa Mashirika na Taasisi za
Umma kuzingatia Maadili ya Viongozi wa Umma katika kutekeleza makujumu
yao.
Katibu Mkuu alisema hayo leo
jijini Dar es salaam wakati wa akifungua mafunzo ya viongozi hao
yalioandaliwa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa
Umma ili kuhakikisha wanaendana Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Mgufuli.
“Maadili yana umuhimu wake mkubwa
katika utawala wa maendeleo ya nchi, kupitia maadili mema wananchi
wanajenga imani na viongozi pamoja na Serikali yao kwa ujumla” alisema
Balozi Mhandisi Kijazi.
Ili kuhakikisha mafunzo yanakuwa
yenye tija, Balozi Mhandisi Kijazi amewasisitiza viongozi hao kutumia
muda vizuri na kujikumbusha na kujifunza maadili hayo kwa manufaa ya
mashirika na taasisi zao pamoja na taifa kwa ujumla.
Balozi Mhandisi Kijazi alitaja
umuhimu wa maadili katika jamii na kusema kuwa yanasaidia kusimamia
rasilimali za umma na kuzitumia kwa maslahi ya wote, kuongeza tija na
thamani ya huduma, zinazotolewa na Serikali, kudhibiti mianya ya
ukiukwaji wa maadili na vitendo vya rushwa, kujenga ujasiri wa
kusimamia Sheria, Kanuni na Taratibu za utumishi wa umma.
Maadili pia yanasaidia wananchi,
viongozi na Watumishi wa Umma kutoa mchango wa haraka katika kutekeleza
maendeleo ya nchi, kuepuka utata wa maamuzi ya migongano ya kimaslahi,
kuwavutia wawekezaji, kujenga na kudumisha amani na utulivu pamoja na
kuondoa na kukomesha ubinafsi kwa viongozi.
Aidha, Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Kijazi amesema kuwa ukiukwaji wa maadili unaathari hasi kwa
taifa ambapo alizitaja baadhi ya athari hizo kuwa ni rasilimali za nchi
kunufaisha wachache, wananchi kukosa haki zao za msingi kutokana na
rushwa na upendeleo, viongozi wa umma kujilimbikizia mali isivyostahili
bila kujali hali za wananchi wanaowaongoza, kupungua kasi ya uwekezaji
pamoja na kudhohofika kwa uchumi wa nchi.
Madhara mengine ya kutojali
maadili ni wananchi kukosa imani na Serikali yao, kuchochea vurugu
pamoja na wananchi kutotii sheria za nchi na hivyo kuhatarisha usalama,
amani na utulivu wa nchi.
Kwa upande wake Kamishna wa
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda
alipokuwa maelezo mafupi kwa Mgeni Rasmi amesema kuwa misingi ya maadili
na maadili yanalenga katika kuzuia mgongano wa maslahi, upendeleo,
matumizi mabaya ya rasilimali za umma na taarifa za ofisi na mwenendo
usiofaa kwa viongozi wa umma ili kuimarisha na kuendeleza dhana za
uadilifu, uwajibikaji na uwazi ambazo ni sifa muhimu za kiongozi.
Ili kuongeza ufanisi katika
utendaji kazi, Jaji Mstaafu Kaganda amesema kuwa ofisi yake inakabiliwa
na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa watumishi ambapo kuna zaidi
ya viongozi 15,000 huku Sekretarieti ina wafanyakazi 200 nchi nzima.
Mafunzo hayo yamehudhuriwa na
washiriki 40 ambapo yalifanyika kwa Mawaziri, Manaibu Waziri, Mkatibu
Wakuu, Manaibu Katibu Wakuu, Wenza wa Viongozi, Wakuu wa Mikoa.
EmoticonEmoticon