Tunaomba radhi sana kwa taarifa kwamba idadi kadhaa ya abiria wetu walishindwa
kufika kwenye maeneo waliyokusudia jioni ya Aprili 2, 2016.
Hii ilitokana na kushindwa kufanya kazi kwa mfumo wa taa kwenye njia ya kurukia kwenye uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro na
hivyo kukosekana kwa usalama ambao ungewawezesha marubani wetu kutua.
Huu ni mfululizo wa matukio ambayo yalisababisha kufutwa kwa ndege mbili
miongoni mwa ndege zetu kutua usiku ule:
miongoni mwa ndege zetu kutua usiku ule:
- Ndege Na. FN157 iliondoka kwenye uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 3.18 usiku ikitarajiwa kutua kwenye
Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro kabla ya muda unaotakiwa saa 4.40 usiku. Wakati ndegte ikikaribia Uwanja wa Kilimanjaro marubani wetu walijulishwa na mnara wa kuongozea ndege kwamba taa zilizopo kwenye njia ya kurukia ndege
zilikuwa hazifanyi kazi lakini hali ingetengemaa muda usiokuwa mrefu. Ndege ilizunguka uwanja wa Kilimanjaro ikisubiri ukarabati wa taa hizo kwa takribani dakika 30 kabla ya kurudi Dar es salaam kwa kuwa taa hizo zilikuwa bado hazifanyi kazi. - Ndege
iliwasili tena Dar es Salaam saa 5.20 usiku na abiria walibaki kwenye
ukumbi wa kusubiria ndege wakati ndege ikijazwa mafuta tena na
marubani wakiandaa mpango mpya wa kusafiri tayari kurudi Kilimanjaro
mapema kadri
iwezekanavyo pindi ukarabati wa taa kwenye njia ya kurukia ndege ukikamilika. Kwa bahati mbaya taa hizo zilikuwa hazifanyi kazi hadi kufikia saa saa 7.00 usiku wa kuamkia Aprili 3, 2016, ambapo muda sahihi na salama kwa marubani wa ndege ukiwa umemalizika kwa kuwa walishakuwa kazini kuanzia saa 12.30 jioni. - Hii inamaanisha kwamba hatukuwa na mbadala wa kufuta safari, na hivyo ndege Na. FN158 ambayo
ilikuwa irudi kutoka Kilimanjaro kuja Dar es Salaam. Abiria wetu waliopata usumbufu walipewa nafasi kwenye ndege iliyokuwa inafuatia na ilisafiri kutoka uwanja wa pili kurudi kule walikotoka. Baadhi ya abira walichukua mbadala huu lakini wengie
waliamua kubaki katika uwanja wa ndege kusubiri ndege iliyofuata. - Abiria wote walioomba kupatiwa usafiri kwenye ndege iliyofuata walisafiri nasi kwa kuelekea maeneo waliyokuwa wanakwenda Aprili 3, 2016.
- Tunaomba radhi kwa abiria wetu waliokuwa kwenye safari ile kwa usumbufu walioupata huku tukiwahakikishia kuwa
tunaweka kipaumbele kikubwa kwenye usalama wa abiria wetu na marubani.
John Corse,
Meneja Mkuu, fastjet
Tanzania
Tanzania
EmoticonEmoticon