Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
akiongea na wananchi katika hospitali ya Rufaa ya St. Francis pamoja na
wajawazito wanaosubiri kujifungua na ambao wapo chini ya uangalizi wa
madaktari.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
amefanya ziara ya siku 1 mjini Ifakara kufuatilia utendaji wa shughuli
mbalimbali za Afya Wilayani Kilombero, Morogoro.
Katika
ziara hiyo, Mhe Ummy ambae alieambatana na Balozi wa Uswisi nchini
Tanzania, Mhe Florence Tonguely-Mattli alifungua kozi ya miezi mitatu ya
kutoa huduma ya dharura ya afya kwa kina mama wajawazito hususani
katika eneo la upasuaji na utoaji wa dawa za usingizi.
Mafunzo
hayo yanayoendeshwa na Taasisi ya Mafunzo ya Kimataifa ya Afya (TTCIH)
chini ya Mradi wa “Upatikanaji wa Uzazi Salama Tanzania” yanawahusisha
Washiriki 70 kutoka mikoa ya Morogoro, Njombe na Mbeya.
Mhe
Ummy pia alikagua shughuli mbalimbali za taasisi za afya ikiwemo
kutembelea Taasisi ya Utafiti ya Ifakara (Ifakara Health Institute),
Hospitali Teule ya Rufaa ya St. Francis, Chuo cha Uunguzi cha Edgar
Malanta na Chuo Kikuu cha Tiba cha St. Francis.
Mhe
Ummy Mwalimu akibadilishana mawazo na Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya
Kimataifa ya Afya (TTCIH) Prof. Pemba, Balozi wa Uswisi nchini Mhe
Florence Tonguely-Mattli.
Picha ya pamoja.
Mhe.
Ummy Mwalimu akiongea na washiriki wakati wa kufungua mafunzo ya miezi
mitatu ya kutoa huduma ya dharura ya afya kwa kinamama wajawazito mjini
katika taasisi ya TTCIF, Ifakara.
EmoticonEmoticon